11 WAFARIKI AJALI ,29 WAJERUHIWA AJALI YA BASI NA LORI MKOANI TANGA LEO

February 11, 2016


VILIO na simanzi vimetawala eneo la Kijiji cha Panga Mlima Kata ya Makole wilayani Muheza mkoani Tanga baada ya kutokea ajali kubwa iliyosabaisha vifo vya watu 11 na majeruhi 29 likihusisha basi la Kampuni ya Simba Mtoto lililokuwa likitokea Tanga kwenda Dar na Lori la Mizigo lililokuwa likielekea mkoani Tanga kupeleka malighafi ya Saruji.

Wananchi waliokuwa wamefurika kushuhudia ajali hiyo wakati wa shughuli
  za uokoaji wa miili ya abiria waliokwama kwenye basi la Simba Mtoto na Lori ikiokolewa walishindwa kujizuia na kujikuta wakibubujikwa na machozi hali iliyopelekea simanzi kubwa.

Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Mihayo Msikhela alithibitisha kutokea
  tukio hilo ambalo lilitokea jana saa moja na dakika hamsini na tano likihusisha basi hilo mali ya kampuni ya Simba Mtoto lenye namba za usajili T.393 DDZ lilikokuwa likiendeshwa na dereva Mwalimu Mbwana likitokea Tanga kwenda Dar na ndipo lilipogongana na lori aina ya semitrella lenye namba za usajili T.738 CFE lililokuwa likiendelea mkoani Tanga. 
Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo kilisababishwa na dereva wqa lori  hilo ambaye alitaka kulipita gari ndogo iliyokuwa mbele yake huku akiwa anasinzia na ndipo aliposhindwa hali iliyopelekea kusababisha ajali hiyo ambayo imeacha simanzi kubwa kwa ndugu na jamaa wa marehemu.

Aliwataja waliofariki dunia kwenye ajali hiyo kuwa ni Fredy

Venance,Mwalimu Mbwana ,Mohamed Saidi na wengine ambapo ni wa familia moja kuwa ni Sada Ally,Nargis Hamis ambaye ni mtoto wa kike mwenye umri wa miaka miwili na nusu  na Raya Said Ally.

Aidha alisema kuwa majeruhi wote 29 ambao kati yao 19 wanaume na
  wanawake 10 wamelazwa kwenye hospitali ya wilaya ya Muheza Teule wakiendelea na matibabu na wawili kati yao wamepelekwa kwenye chumba cha upasuaji na wanne wamepekwa ICU.     “Lakini pamoja na hilo nitoe wito kwa madereva kuchukua hatua stahiki za kupumzika ili wanapokuwa barabarani waweze kufanya kazi zao kwa ueledi mkubwa ili kuepukana na ajali wanazoweza kuziepuka kwani hili la leo ni uzembe wa dereva wa lori “Alisema RPC Mihayo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »