WADAU WA UFUGAJI,KILIMO NA UVUVI WAKUTANA NA KUTOA MAONI YA UCHAMBUZI WA MWONGOZO WA KUANDAA MPANGO NA BAJETI YA SERIKALI YA MWAKA WA FEDHA 2016/17

February 11, 2016

Wakulima wadogo wadogo zaidi ya 45  katika harakati za maendeleo nchini na  sekta za uvuvi, na ufugaji kutoka mikoa mbalimbali nchini wamekutana jijini Dar es salaam katika kujadili mwongozo wa kuandaa mpango na bajeti ya serikali 2016/2017.

Warsha hiyo ambayo imeandaliwa  na ushirikino wa mashirika matano ambayo ni  Oxfam, Policy Forum, ANASAF, Action Aid na TGNP zaidi ikiwa ni kuwaleta pamoja wakulima hao wadogowadogo  katika kupitia mwongozo na kuujadili kwa ukaribu pamoja na kuuchambua kwa kina zaidi.

Wakati akitoa majumuisho kutoka ukurasa wa 14-20 Bi Flora Mathias Kutoka Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkulima mdogo ameomba Mkulima ameiunga mkono hoja ya mwanamke kuthaminiwa na kupata nafasi ya kuuza Bidhaa zake, kupewa nafasi ya kujitambua na kumiliki Ardhi, huku akiulalamikia mwongozo huo wa bajeti elekezi kutoweka wazi kuhusu mfuko wa wanawake katika kusaidia uzalishaji na kuomba bajeti inayokuja izingatie hilo.

Mzee Namagono Hassan kutoka kundi la wakulima ametoa  maelezo kutoka ukurasa wa 6-9  kuhusu mambo muhimu katika mwongozo wa Bajeti 2016/17, kuwa pamoja na kuanzishwa kwa Benki ya wanawake, isitazame tuu wanawake wa mjini bali na  vijijini kwani wao ndio wazalishaji zaidi wa Chakula kuliko waishio mijini.

Kwa upande wake Datius Pastory Inshansha Mwanaharakati na Mkulima mdogo ukurasa wa 20-23 amepitia ukurasa 23-24 unaotoa maelekezo mahsusi kwa sekretarieti za mikoa na mamlaka ya serikali za mitaa na kushauri kuwepo uwazi wa mapato na matumizi ya Serikali za Mitaa, pia Bajeti ielekezwe zaidi vijijini kulipo mjini na kudhibiti fedha za uvuvi,kilimo na ufugaji zisiishie kwa watu wachache bali wahusika kwa ujumla.

Maelezo mengine yametolewa na Bwana Adam Simwinga kuhusu ukurasa wa 9-15 kipengele cha Maelekezo ya Maandalizi ya bajeti kwamba amegundua hakuna mkakati wa kuongeza mapato kupitia simu, mkakati wa msamaha wa kodi, hivyo wameshauri kilimo kiwe ni sehemu ya eneo wezeshi na malighali katika viwanda nchini Tanzania na katika mpango wa maendeleo na kuongeza kuwa asilimia 30% hazijitoshelezi kukuza sekta ya kilimo nchini.

Wanaharakati hao wameishauri serikali kutowasahau katika kuwawezesha mikopo ili kukuza sekta zao kimaendeleo huku wakilalamika wakulima  kutoshirikishwa kikamilifu.

“Tunaomba mkopo wa Magari ya wabunge upungue kutoka Mil 90 hadi Mil 20 ili zile mil 70 zitumike katika shughuli zingine za maendeleo ikiwemo na kilimo na pia kuwe na viwanda vidogo vidogo katika mikoa mbalimbali mfano kiwanda cha Machungwa” aliongeza Bi. Kidani Mhenga wanajadili ukurasa wa 3-5 mapitio ya uchumi na utekelezaji wa Bajeti

 Bi. Kidani Mhenga kutoka kikundi namba tatu ambao walikuwa wanajadili ukurasa wa 3-5 mapitio ya uchumi na utekelezaji wa Bajeti za Serikali kuoka katika mpango wa bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2016/2017 
Mzee Namagono Hassan Kutoka kikundi namba moja akitoa maelezo kutoka katika mwongozo wa kuandaa mpango wa bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2016/2017 kutoka ukurasa wa 6-9  unaoelezea mambo muhimu katika mwongozo wa Bajeti 2016/17 
 Bi Flora Mathias Kutoka Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkulima mdogo akitoa majumuisho kutoka kipengele cha namna ya kudhibiti Bajeti za Serikali kutoka katika mwongozo wa kuandaa mpango wa bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2016/2017 ukurasa wa 14-20, picha ya juu ni wanakundi wakiwa wanajadili swala hilo. Picha ya juu ni baadhi ya mama Shujaa wa chakula ambao wanatoka katika Kampeni ya Grow inayoendeshwa na Oxfam Tanzania pamoja na wadai wengine wa kilimo
Bwana Adam Simwinga akitoa maelezo kutoka kundi namba mbili ambao walikuwa wachambua mpango wa bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2016/2017 ukurasa wa 9-15 kipengele cha Maelekezo ya Maandalizi ya bajeti
 Datius Pastory Inshansha ambaye ni Mwanaharakati na Mkulima mdogo mdogo akiwasilisha kundi lake la Tano ambao walikuwa wanajadili ukurasa wa 20-23 kutoka katika mwongozo wa kuandaa mpango wa bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2016/2017 inayozungumzia maelekezo mahsusi kwa sekretarieti za mikoa na mamlaka ya serikali za mitaa.
Baadhi ya wakulima, wafugaji na wavuvi wakiendelea namjadala 

Picha na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa



Share this

Related Posts

Previous
Next Post »