Waziri Mkuu, Kassim Majliwa
akionyeshwa na kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamla ya bandari Tanzania,
Mhandisi Aloys Mtei eneo zinakotia nanga meli kubwa zinazoleta mafuta
nchini kupitia bandari ya Dar es salaam Februari 11, 2016. (Picha na
ofisi ya Waziri Muu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akitaka maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo na Mizani,
Bibi Magdalena Chuwa (kulia) kuhusu sababu zilizomfanya azuie matumizi
ya flow Meter katika kuhakiki kiwango cha mafuta yanayoingia nchini
kupitia bandari ya Dar es salaam wakati alipofanya ziara kwenye badari
hiyo Februari 11, 2016. katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Raymound
Mushi. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua eneo ambalozo mafuta hufunguliwa na kufungwa ili kwenda kwenye
matangi ya kuhifadhia mafuta ya makampuni mbalimbali yanayoagiza mafuta
toka nje ya nchi wakati alipokwenda enero la Kigamboni jijini Dar es
salaam kuonamianya inayotumika kukwepa kodi za mafuta yanayoagizwa nje
ya nchikupitia bandari ya Dar es salaamFebruari 11, 2016. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua flow Meter ya Mafuta ya kupikia ambayo matumizi yake yalizuiwa
na Wakala wa Vipimo na Mizani kwa madai kuwa ilikuwa na kasoro . Wapili
kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakla wa Vipimo na Mizani, Magdalen Chuwa.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WaziriMkuu, Kassim Majliwa
akikagua ujenzi wa Flow Meter eneo la Kigamboni jijini Dar es salaam
Februari 11, 2016. Mtambo huo utatumika kupima wingi wamafuta yanayotoka
kwenye meli na kuingizwa hapa nchini. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya
Ilala Raymound Mushi. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua eneo lenye mabomba yanayotumika kupitisha mafuta kutoka kwenye
meli kupitia bandari ya Dar es slaam wkatia lipofanya ziara ya kukagua
miundombinu yenye mianya ya ukwepaji kodi hasa kwenye mafuta yanayoingia
nchini Februari 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………………………………………………..
*Aibukia kitengo cha mita za kupimia mafuta Kurasini
*Akuta mafundi wakizitengeneza, akuta zimejaa kutu
*Ataka barua ya maelezo ifikapo saa 11 leo jioni
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amefanya ziara ya ghafla kwenye kitengo cha upimaji mafuta bandarini
(Oil Flow Metres) na kukuta zimejaa kutu baada ya kutelekezwa kwa miaka
zaidi ya mitano. Pia alitembelea mita za kupimia mafuta zinazoendelea
kujengwa Kigamboni.
Aidha, Waziri Mkuu amempa saa nne
tu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo nchini (WMA), Bi. Magdalena Chuwa
aandike barua ya kujieleza ni kwa nini aliamua kufunga mita hizo
zisitumike kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita na amletee barua hiyo
ofisini kwake ifikapo saa 11 leo jioni.
“Nataka unieleze ni kwa nini
ulitoa maelekezo ya kufunga mita hizo, na kwa nini jana uliamua kubadili
uamuzi huo? Ni kwa nini umeamua kuchukua maamuzi haya baada ya kupokea
ujumbe wa simu ya mkononi (sms) wakati mita zimekaa bila kufanya kazi
kwa miaka mitano? Ni kwa nini umeamua kufanyia kazi ujumbe wa sms wakati
unajua Serikali inafanya kazi kwa maandishi rasmi?” alisema Waziri
Mkuu.
“Umesema mlikuwa mnatumia
utaratibu wa kupima kwa kijiti. Huu hauna uhakika na huwezi kutegemea
taarifa ya mtu mwingine au kuingia kwenye meli ya mtu na kuanza kuchukua
vipimo hadi ujiridhishe. Nataka kujua ni kwa nini mlikuwa na utaratibu
wa ku-bypass mafuta ili yasipite kwenye mita za kupimia mafuta? Ni kwa
nini umetoa amri zianze kutengenezwa jana na siyo mwaka 2012 au 2013?”
alihoji Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu alisema mita hizo za
Kurasini zilinunuliwa na Serikali kwa gharama za dola za marekani
milioni 1.2 (wakati huo) na haiwezekani kuacha kuzitumia wakati watu
wanachezea mifumo na kuongeza mianya ya kupoteza mapato kwa Serikali.
Ameagiza mita hizo zianze kufanya kazi mara moja.
Wazir Mkuu alisema matumizi ya
mita hizo yaliafikiwa na Serikali baada ya kubaini upotevu mkubwa wa
kodi kwenye mafuta yanayoingizwa nchini na baada ya kuona hakuna tija ya
kuendelea na ukadiriaji au kupokea taarifa za waagizaji peke yao.
Waziri Mkuu ambaye aliwasili
Kurasini leo saaa 4: 30 asubuhi (Alhamisi, Februari 11, 2016) kwenye
kitengo hicho kilichopo Kurasini (Kurasini Oil Jetty), alikagua mita
hizo na kisha kwenda kukagua meli iliyokuwa ikishusha mafuta bila
kutumia mita hiyo ya kupima mafuta yanayopokelewa kwa sababu mafundi
walikuwa bado wanaendelea na ukarabati.
Akiwa Kurasini, Waziri Mkuu
alielezwa na Bibi Chuwa kwamba mita hizo zilianza kufanyiwa ukarabati
jana na leo asubuhi moja imekamilika ambayo ni ya kupokelea mafuta ya
petroli. Ya dizeli ilikuwa inafunguliwa na mafundi na kukutwa imejaa
kutu sababu ya kutotumika kwa muda mrefu.
“Hii ya dizeli imefunguliwa leo
na ile ya mafuta ya kula, haijawahi kufanya kazi tangu ilipofungwa mwaka
2011,” alielezwa Waziri Mkuu na Kaimu Mkurugenzi wa Bandari, Eng.
Aloyce Matei.
Alipoulizwa ni kwa nini aliamua
kuzifungia mita hizo ziisifanye kazi, Bi. Chuwa alijibu kuwa alifikia
uamuzi huo baada ya kupokea malalamiko kwamba zinawapunja wateja. Hata
hivyo, hakufafanua ni wateja gani au wa aina gani.
Katika hatua nyingine, Waziri
Mkuu Majaliwa, ametembelea na kukagua mita mpya za kupimia mafuta ambazo
zinajengwa Kigamboni. Mita hizo zimegharimu dola za marekani milioni 6
(sawa na sh. bilioni 12.96/- za sasa).
Akiwa hapo, Waziri Mkuu alielezwa
kwamba ujenzi huo ambao ulianza miezi nane iliyopita, unatarajiwa
kukamilika ifikapo katikati ya mwezi Machi, 2016. “Tunajitahidi kazi hii
ikamilike ifikapo katikati ya mwezi ujao,” alisema Eng. John Bura,
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya BQ Contractors Ltd ambayo inasimamia
ujenzi wa mita hizo.
Vilevile, Waziri Mkuu alitembelea
sehemu ya kuchukulia mafuta yanayotoka bandarini (TPA Manfold) iliyoko
Kigamboni na kukagua mitambo ya kusambazia mafuta kwenye matenki ya
mafuta ya kampuni ya TIPER yaliyoko Kigamboni yanayomilikiwa kwa ubia
bainaya Serikali na kampuni ya Oryx Energies.
Katika ziara hiyo ilibainika kuwa
Kampuni ya TIPER imejiunganishia bomba la moja kwa moja kutoka kwenye
bomba kubwa la mafuta linalotoka bandarini hali iliyomlazimu Waziri Mkuu
kuagiza kwamba bomba hilo litolewe kwenye maungio hayo ndani ya mwezi
mmoja.
“Natoa mwezi mmoja hili bomba
liondolewe kwenye mfumo huu na kama yapo mabomba mengine pia
yaondolewe,” alisema huku akionyesha karatasi iliyokuwa mfukoni kwake
yenye mchoro unaobainisha kuwa kuna bomba jingine la inchi 10 limeungwa
kinyemela kwenye bomba kuu.
“Kila mmoja anapaswa aje kuchukua pale kwenye manfold
ili tujue nani kachukua nini. Msajili wa Hazina hili ni eneo lako na
wewe unamiliki TIPER kwa asilimia 50, hebu simamia hili. Ninyi TPA
leteni mapendekezo yenu Serikalini ili tuone tunaweza kudhibiti vipi
vitendo kama hivi,” alisema Waziri Mkuu.
Pia alimtaka Msajili wa Hazina,
Bw. Lawrence Mafuru awasiliane na Mwanasheria Mkuu ili waangalie upya
mkataba na umiliki wa matenki hayo uwe chini ya Serikali kwa asilimia
100 ili mafuta yanayoagizwa na Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja
(Petroleum Bulk Procurement Agency) yaweze kuhifadhiwa huko.
Mapema, Waziri Mkuu ambaye alifuatana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, alikagua eneo lamanfold ya Mamlaka ya Bandari iliyopo Kigamboni na kukuta ni kampuni nne tu zenye matenki Kigamboni ambazo zinachukua mafuta yao hapo.
Kampuni hizo ni HASS, WORLD OIL,
LAKE OIL na MOIL. TIPER haikutaka kufuata mfumo huo licha ya kuwa nafasi
ya kufanya hivyo ipo. Kampuni nyingine zenye matenki yake nchi kavu,
zinachukulia mafuta kwenye manfold ya Kurasini.
EmoticonEmoticon