Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Rais
mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Kenya (FKF), Nick Mwendwa
kwa kuchaguliwa kuliongoza shirikisho hilo.
Katika salamu hizo, Malinzi
amempongeza Mwendwa kwa nafasi hiyo aliyopewa kuliongoza soka la nchini
Kenya, na kuahidi TFF itaendelea kushirikiana nae katika maendeleo ya
mpira wa miguu kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Nick Mwendwa alishinda nafasi
hiyo jana katika uchaguzi uliofanyika jijini Nairobi kwa kupata alama 50
kati ya 77 za wapiga kura wote na kupata nafasi hiyo iliyokua
inashikiliwa na Samwel Nyamweya aliyemaliza muda wake.
EmoticonEmoticon