Ngoma yake ya Kwanza inaitwa AMBERA, ni ngoma tamu japo haikufanya vizuri kutokana na upya wake kwenye game. Hiyo haikumkatisha tamaa na sasa ameachia ngoma ya pili ijulikanayo kama INDE MONI.
Huyu si mwingine bali ni msanii wa kizazi kipya mwenye miondoko ya dansi aitwae Zomboko Jonus a.k.a ZOMBO (Pichani) kutoka Jijini Mwanza.
"Wimbo wa kwanza haukufanya vizuri ila kwa wimbo huu wa pili nina matumaini makubwa kwamba utapokelewa vyema na mashabiki wa muziki nchini". Alisema Zomboko wakati akizungumza na BMG kuhusiana na ujio wa wimbo wake huo uitwao Inde Moni ambao amefanya katika Studio ya Viber Nation iliyopo Jijini Mwanza chini yake Producer An Whyle.
Zombo alisema wimbo huo umetambulishwa rasmi katika Mitandao ya Kijamii na kwamba anajiandaa kwa ajili ya kuanza kuutambulisha katika vituo mbalimbali vya radio hapa nchini ambapo alitanabaisha kwamba utambulisho huo utaanzia Jijini Mwanza.
BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA
Na George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group-BMG
EmoticonEmoticon