Naibu Waziri Ofisi ya Makamu Rais Muungano na Mazingira Atembelea Ujenzi wa Mtaro Uwanja wa Mnazi Mmoja na Jangombe Eneo Ilikozama Nyumba.

February 11, 2016

Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akitembelea Ujenzi wa Mradi wa Mtaro katika Uwanja wa Mpira Mnazi Mmoja akiwa katika ziara zake Zanzibar kutembelea Miradi ya Mazingira inayosimamiwa na Muungano.akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Mhe Hamad Yussuf Masauni. 
Kijicho cha Kampuni ya Ujenzi Mtaro huo kikiwa kazini katika uchimbaji wa mtaro huo nyambu ya pili pwani ya kizingo Zanzibar. 
Makalbi ya mtaro wa kupitishia maji kutoka katika viwanja vya mpira mnazi mmoja yakitandikwa, na kulia ni mabomba ya mtaro huo ya zamani yaliokuwa yakitoa huduma hiyo ya kupitisha maji kutoka katika uwanja huo. 
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe.Luhaga Mpina akiangalia ujenzi huo wakati wa ziara yake kutembelea miradi huo. 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akimsikiliza Mhandisi wa Baraza la Manispa Zanzibar Ndg Mzee Khamis Juma akitowa maelezo ya kitaalumu ya Ujenzi wa Mtaro wa maji machafu wakati wa mvua kunyesha

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »