Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, akizungumza na Maafisa wa Jeshi la
Polisi, wakati wa mkutano wa Kujitambulisha na kufahamiana na Watendaji
wakuu na Maafisa wa Jeshi la Polisi uliofanyika Makao Makuu ya Jeshi
hilo, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Mngodo alilipongeza
jeshi hilo kwa kusimamia Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu. Kulia kwa
Katibu Mkuu ni Inspekta Jenerali wa Jeshi hilo (IGP), Ernest Mangu.
Inspekta Jenerali wa Jeshi la
Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu (kushoto) akiwaongoza watendaji wakuu
na maafisa wa jeshi hilo kuimba wimbo wa maadili wa jeshi hilo wakati wa
ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John
Mngodo (wapili kushoto). Ziara hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya jeshi
hilo jijini Dar es Salaam leo, ilikuwa na lengo la kujitambulisha na
kufahamiana na watendaji hao. Watatu kushoto meza kuu ni Naibu IGP,
Abdulharam Kaniki, wapili kulia ni Kamishna wa Lojistiki na Fedha wa
Jeshi la Polisi Clodwig Mtweve, na kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, akizungumza na Watendaji wakuu na
Maafisa wa Jeshi la Polisi nchini wakati alipofanya ziara Makao Makuu ya
Jeshi hilo jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la kujitambulisha na
kufahamiana na watendaji hao. Kushoto meza kuu ni Inspekta Jenerali wa
Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu, Watatu kushoto meza kuu ni
Naibu IGP, Abdulharam Kaniki, wapili kulia ni Kamishna wa Lojistiki na
Fedha wa jeshi hilo, Clodwig Mtweve, na kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova.
Inspekta Jenerali wa Jeshi la
Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu (kushoto) akitoa taarifa ya Jeshi hilo
wakati wa Ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, John Mngodo, alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es
Salaam kwa lengo la kujitambulisha na kufahamiana na watendaji wa jeshi
hilo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (kulia), akiagana na Kamanda wa
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova baada ya
kumaliza ziara yake katika Makao Makuu ya jeshi hilo jijini Dar es
Salaam. Katikati ni Kamishna wa Lojistiki na Fedha wa jeshi hilo,
Clodwig Mtweve, wapili kushoto ni Kamishna wa Polisi Jamii nchini, Musa
Ali Musa, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai,
Diwani Athumani.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo ( watano kulia), Inspekta Jenerali
wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu (watano kushoto) wakiwa
katika picha ya pamoja na Watendaji wakuu na Maafisa wa jeshi hilo muda
mfupi baada ya kumaliza ziara ya kutembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo
jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
EmoticonEmoticon