Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), kwa kushirikiana na
mzabuni wa tenda ya elektroniki benki ya CRDB, leo limetangaza tenda ya
kumsaka mshauri wa mfumo wa Elektroniki (Consultant) kwa ajili ya
kupitia mapungufu yaliyopo katika mfumo wa uuzaji tiketi wa elektroniki
katika michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania.
TFF imetangaza tenda hiyo ili kumpata mshauri wa mfumo huo wa tiketi
za elektroniki, ambao ulisamishwa na serikali mapema mwaka huu mwezi
Aprili. Maombi ya tenda yawasilishwe katika ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF
zilizopo Karume jijini Dar es salaam, kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 10
jioni siku za kazi Jumatatu mpaka Ijumaa. Gharama ya fomu ya kuombea tenda ni shilingi laki moja (100,000), na mwisho wa maombi ni Disemba 17, 2015.
EmoticonEmoticon