NAMNA MBUNGE MTEULE WA JIMBO LA TANGA,MUSSA MBARUKU ALIVYOFANYA ZIARA KWENYE MAENEO YALIYOAPATWA MA MAFURIKO YA MVUA

November 17, 2015



MBUNGE Mteule wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku amewataka watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kuacha kukaa ofisini badala yake waende kwenye maeneo ya wananchi waliokumbana na mafuriko kutokana na mvua zinazonyesha juzi jijini Tanga na kusababisha maji kutuama katika makazi yao.

Mbaruku alitoa wito huo jana wakati alipofanya ziara ya kushtukiza
katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa iliyonjesha hivi karibuni jijini Tanga na kuathiri baadhi ya maeneo yalisiyokuwa na miundombinu imara ya kupitisha maji.

 
Maeneo ambayo alitembelea ni Kwanjeka, Shule ya Msingi Mnyanjani na eneo la Jengo la Hospitali la Kata ya Mnyanjani na shule ya Msingi Magaoni Kata ya Magaoni ambapo katika ziara hiyo alibaini kuwepo changamoto mbalimbali ikiwemo tatizo la kutokuwepo miundombinu imara inayosababisha maji kujaa maeneo ya watu nyakati za mvua.
 
Alisema kuwa kimsingi watendaji wa halmashauri hawawezi kuendelea kukaa ofisini wakati wananchi wa maeneo hayo wanateseka na tatizo la maj kujaa kwenye maeneo yao bila kupatiwa ufumbuzi wa kina hali iliyopelekea kushindwa kutambua wafanye nini.
 
Aidha akiwa kwenye eneo lililoathirikana mafuriko hayo alijaribu
kuwasiliana na Mhandisi wa Jiji la Tanga ambapo alimtaka kufika kwenye maeneo yote yaliyoathirika na tatizo hilo ili kuangalia namna ya kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo.

  “Hali hii sio nzuri kabisa kwa sababu ikiendelea hivi bila kuwepo
kwa utatuzi wake wananchi wanaweza kukumbana na magonjwa mbalimbali ya milipuko ikiwemo Kipindupindu na mengineyo hivyo niwatake watendaji wa Halmashauri hasa ofisi ya Mhandisi wa Jiji la Tanga kuhakikisha wanalishughulikia tatizo hili haraka “Alisema Mbunge huyo.

Aliongeza kuwa afya za wananchi ni muhimu sana kwa ajili ya ukuaji wa maendeleo yao ya kila siku na kuchangia ukuaji wa uchumi hivyo ni muhimu wao kuweza kuwekewa miundombinu imara itakayowezesha maji yanayofika kwenye maeneo yao nyakati za mvua yaweze kupita kuelekea baharini ili kuondoa adha hiyo kwao.

Hata hivyo alisema suala kubwa atakalokwenda kulifanyia kazi ni
kuhakikisha maeneo hayo yanayoathiriki na tatizo la kuwepo kwa
mafuriko mara kwa mara nyakati za mvua atahakikisha anaweka
miundombinu imara kwa kujenga mifereji itakayoweza kupitisha maji yatakayoweza kuungana na mingine kwa ajili ya kupeleka maji hayo baharini.

 
Akiwa shule ya msingi Mnyanjani alibaini kuwepo kwa changamoto kubwa ya wanafunzi kushindwa kuhudhuria masomo hasa kipindi cha mvua kubwa zinapokuwa zikinyesha kutokana na kuwepo mrefeji mkubwa ambao unapofurika maji yake huwa ni hatari kwa wanafunzi wanaosoma shule hiyo.  

Akizungumza wakati alipomkaribisha Mbunge huyo alipoingia shuleni hapo,Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,Edna Sariko alimueleza mbunge huyo kuwa tatizo la kutokuwepo mifereji kwenye maeneo hayo kumesababisha maji kujaa kwenye daraja lililopo karibu na eneo la shule hiyo na kusababisha wanafunzi kushindwa kuhudhuria masomo pindi mvua zinapokuwa zikinyesha.
 
Hata hivyo Mbunge huyo alihaidia kuzichukua changamoto hizo na kwenda kuzifanyia kazi kwa upana ili walimu na wanafunzi waweze kuondokana na kero hiyo ambayo imekuwa ikimwamisha juhudi za kuinua kiwango cha elimu shuleni hapo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »