Meneja
Mawasiliano wa Tigo, John Wanyanja, akizungumza na waandishi wa habari
wakati akimkaribisha Meneja Mkuu wa Tigo kuzungumza na wanahabari.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wakati wa uzinduzi wa chapa
mpya yenye kauli mbinu ya ‘Live it, love it’ itakayoimarisha nafasi ya
mbunifu anayeongoza kwa ubunifu wa kidigitali nchini. Kulia ni Meneja
Chapa wa Tigo, William Mpinga.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez, akionesha simu mpya zenye menyu ya Kiswahili wakati wa mkutano huo.
Meneja
Chapa wa Tigo, William Mpinga (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Masoko wa Tigo, Olivier Prentout.
Mkurugenzi
wa Huduma za Masoko wa Tigo, Olivier Prentout (kulia), akizungumza na
wanahabari kuhusu huduma mpya za Tigo kuelekea Sikukuu ya Krismas.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea.
……………………………………………………………………….
Mwandishi Wetu
KAMPUNI
ya Mawasiliano ya Tigo, imezindua chapa mpya yenye kauli mbinu ya ‘Live
it, love it’ itakayoimarisha nafasi ya mbunifu anayeongoza kwa ubunifu
wa kidigitali nchini.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa chapa hiyo Dar es Salaam leo asubuhi, Meneja Mkuu
wa kampuni hiyo, Diego Gutierrez alisema chapa hiyo mpya itahakikisha
inakuwa rafiki nzuri kwa Watanzania kuziona ndoto zao na kuzifikia.
Alisema
kwa hapa nchini kama zilivyo nchi zingine intaneti imekuwa nisehemu
muhimu ya maisha ya watu kutokana na huduma za kidigitali kutumika
katika biashara, elimu, kwa familia na kwa kujiburudisha.
“Tumejikita
kwenye utoaji huduma katika matarajio hayo na rekodi ya mwenendo wa
ubunifu wetu unatupa imani kuwa tunafanikiwa,” alisema Gutierrez.
Katika
hatua nyingine, kampuni hiyo imetoa ofa kwa wateja wake kwa kuuza simu
ya smartphone ya aina ya Tecno Y3 kwa sh. 99,000 kuelekea msimu wa
Sikukuu ya Kristmass na Mwaka Mpya.
Gutierrez
alisema simu hiyo itakuwa na ‘menu’ ya Kiswahili itakayomuwezesha mteja
kuitumia kwa urahisi huku ikiwa na kamera mbele na nyuma, betri
linalokaa kwa muda mrefu na vitu vingine.
EmoticonEmoticon