Waziri Binilith Mahenge akutana na Balozi wa Sweden . Katarina Rangnitt DAR ES SALAAM

October 12, 2015

1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Mheshimiwa Binilith Mahenge akiukaribisha ujumbe wa Mabalozi waliotembelea Ofisini kwake wakiongozwa na Balozi wa Sweden Bi. Katarina Rangnitt Ujumbe huo ulifika kwa ajili ya kuzungumzia maswala ya mabadiliko ya Tabia Nchi kwa Nchi za zinazoendelea.
2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Mheshimiwa Binilith Mahenge akiongea jambo na Balozi wa Sweden Bi. Katarina Rangnitt aliyeongoza Ujumbe wa Mabalozi waliofika Ofisini kwake Oktoba 12, 2015.
3
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Mheshimiwa Binilith Mahenge akimsikiliza Balozi wa Uturuki Nchini Tanzania Bi. Yasemin Eralp aliyekuja Ofisini kwake kujitambulisha.
4
Balozi wa Uturuki Nchini Tanzania Bi. Yasemin Eralp akisaini kitabu cha Wageni mara baada ya kumtembelea Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Mheshimiwa Binilith Mahenge Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »