Siku Nane zatolewa kuhakiki taarifa kituo cha kupigia kura

October 12, 2015

index 
Na Anitha Jonas-Maelezo Dar es salaam
………………………………………………….
Tume ya Taifa ya Uchaguzi  yawaasa  wapiga kura kote nchini kuhakiki taarifa zao katika vituo vya vya kupiga kura siku nane kabla ya uchaguzi.
Hayo yamesema jana  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva alipokuwa akizungumza katika mkutano na viongozi wa vyama vya siasa uliyofanyika Oktoba 12, 2015  jijini Dar es Salaam,
Jaji Lubuva amesema kuwa lengo la mkutano huo ni  kushauriana na vyama vya siasa katika kuelekea siku ya uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba 25 mwaka huu.
“Tume imepanga kuhakikisha kila mpiga kura mwenye sifa ya kupiga kura  anapata haki ya kupiga  kura na imeagiza wasimamizi wa kura kutoa nafasi za upendeleo kwa watu wenye ulemavu  wa aina mbalimbalina na imeandaa karatasi maalum za kupigia kura kwa watu wenye walemavu wa kuona”,alisema Jaji Lubuva.
Aidha Jaji Lubuva aliwasihii viongozi hao kunadi sera zao majukwaani badala ya kuilalamikia Tume katika majukwaa  wakati wa kampeni  pia amewasaa wanasiasa hao  kupeleka malalamiko yao katika ofisi husika na kuacha kukimbilia waandishi wa habari.
Mbali na hayo Mwenyekiti wa Tume hiyo aliendelea kusisitiza juu ya viongozi wa vyama vya siasa wanao walazimisha wapigia kura kubaki katika vituo vya kupigia kura kuacha kauli hizo kwani kwa uzoefu unaonyesha kwamba wafuasi wa vyama wanapokutana pamoja huweza kuchangia uvunjifu wa amani.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw.Kailima Ramadhani alisema Tume ilibani kuwa jumla ya watu 3,870 walioandikishwa hawakuwa raia wa Tanzania na hivyo vitambulisho vyao vimerejeshwa Tume na taarifa zao kufutwa kwenye kanzidata ya daftari la kudumu la kupiga kura.
“Katika kuelekea uchaguzi  Tume imeandaa vituo vya kupigia kura 65,105 ambapo Tanzania Bara ni vituo 63,525 na Zanzibar  ni vituo 1,580 kila kituo kitakuwa na uwezo wa kuhudumia wapiga kura 450 na kituo kitakacho kuwa na wapiga kura zaidi ya 500 kitagawanywa katika vituo viwili,”alisema Bw.Ramadhan.
Mpaka sasa tume imeshasambaza vifaa mbalimbali vya uchaguzi nchini, vifaa ambavyo havijasambazwa ni pamoja na karatasi za kura, wino maalumu, karatasi za matokeo na muhuri wa kituo kutokana na umuhimu wake ila vinatarajiwa kuisambazwa hivi karibuni.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »