WILAYA YA TANGA YAFANIKIWA KWA KIASI KIKUBWA KWENYE SEKTA YA ELIMU.

January 07, 2014
Na Mbaruku Yusuph,Tanga

WILAYA ya Tanga katika mwaka huu wa 2013 mefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika sekta ya elimu kwa ufaulu wa wanafunzi wa  darasa la saba ambao walifanya mtihani wao wa Taifa mwezi wa kumi  ukilinganisha na matokeo ya mwaka jana.

Akizungumza ofisini kwake kaimu Afisa elimu Jiji, Damas Kifanga alisema kuwa ufaulu huo uliojumuisha shule 93 za Tanga mjini na Vijijini  umeongezeka mwaka huu ingawa sekta hiyo ya elimu inakabiliwa na changamoto nyingi.

Aidha alisema katika sekta hiyo ya elimu Wilaya ya Tanga mwaka huu imefanikiwa kutoa wanafunzi 4266 kati ya wanafunzi 6261 sawa na 40% ya ufaulu wa matokeo ya darasa la saba ambapo ni tofauti na mwaka jana kitu ambacho kinaleta hamasa katika sekta hiyo muhimu katika maisha ya kila siku.

Hata hivyo Kifanga alisema kuwa ili kukabiliana na idadi ndogo ya wanafunzi waliokosa nafasi za kujiunga na shule za serikali,ni lazima kuunganisha nguvu kutoka serikalini,wazazi na taasisi zisizo za kiserikali ili kuweza kuinua sekta hiyo ya elimu katika Wilaya ya Tanga Mjini.


Alisema kuwa upo umuhimu wa utolewaji wa chakula mashuleni ili kuboresha mahudhurio na kuwepo na usikivu mzuri wa wanafunzi pindi wawapo madarasani kitu ambacho bado kinasuasua kwa baadhi ya shule na kupelekea kufikia malengo mazuri waliojiwekea.

Kifanga alizidi kusema kuwa uboreshwaji wa mindombinu ni muhimu katika sekta hiyo ili kupunguza msongamano wa wanafunzi katika baadhi ya shule kitu ambacho kwa namna moja au nyingine kinaweza kupunguza umakini kwa wanafunzi wawapo katika masomo yao.

Bwana Kifanga alitumia fursa hiyo kuiomba serikali kuongeza jitihada katika utowaji wa fedha za uwendeshaji wa shughuli zote za elimu na kuwa saidia kukamilisha  kwa wakati miundombinu amabyo wananchi wanayanzisha kwa nguvu zao katika kuboresha elimu Wilayani humu.

Ameiomba serikali kuwa  Halmashauri  zinapaswa kuboreshewa uewzo wa kifedha  ili kuweza kusaidia mafunzo ya walimu waliopo makazini ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi wa kielimu.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »