News kutoka Mahakamani, Hukumu ya Zitto Kabwe sasa kesho saa nane mchana
HABARI kutoka Mahakamani zinasema kuwa Mahakama Kuu imeahirisha hukumu
ya Zitto Kabe dhidi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo iliyopangwa
kutolewa leo asubuhi. Taarifa hizo zilizidisha chungu na tamu kwa pande
zote mbili juu ya wafuasi wa Zitto na viongozi wengine wa Chadema.
Zitto Kabwe.
imewekwa Januari 6 saa saba na nusu mchana.
Kwa mujibu wa taarifa za awali kwa watu waliokuwa mahakamani hapo, kesi
hiyo sasa hukumu yake itasomwa kesho saa nane mchana. Kesi hiyo ni
mwendelezo wa mgogoro mkubwa wa Chadema dhidi ya Kabwe anayedai kuwa
hiyo ni vita ya ukombozi dhidi ya wahafidhina kwenye chama chao.
Jana katika mitandao ya kijamii walikuwa wakirushiana makombpra ambapo Zitto alionekana kumjibu Tundu Lissu kama ifuatavyo.
chanzo:Handeni kwetublogspot.com
Jana katika mitandao ya kijamii walikuwa wakirushiana makombpra ambapo Zitto alionekana kumjibu Tundu Lissu kama ifuatavyo.
"Lissu anasema nimepewa magari 2 na Mzee Mkono. Anasema kaambiwa na Mkono. Naamini Mkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa Freeman Aikaeli Mbowe tshs 40m ili Mbowe asifanye kampeni Musoma vijijini.Nadhani alimwambia pia mwaka 2008 (baada ya orodha ya mafisadi kutangazwa 2007) Mkono alimpa Freeman tshs 20m za uchaguzi wa Tarime na Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa. Nadhani alimwambia pia kuwa Mwaka 2010 Mkono alimpa Mbowe tshs 200m za kampeni ya Slaa.Pia hakusahau kumwambia kuwa Rostam Aziz alimpa Mbowe tshs 100m za kampeni. Lissu anajua kuwa gazeti la Tanzania Daima limeanzishwa na fedha za chama kutoka Conservative Party?
Nimefanya internship yangu kwa Mkono and Company Advocates kuhusu masuala ya mikataba. Mzee Mkono ni Mzee wangu na alisaini petition ya kumtoa Waziri Mkuu Pinda.Lissu awaambie waliyemtuma wamwambie ukweli wote. Lissu ajue yeye ni kifaranga tu, Mimi namtaka mama wa kifaranga ajitokeze. Aeleze aliingia deal gani na Kinana na Sumaye mwaka 2005 kufuatia deni lake NSSF. Aweke wazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba ya Umma ilipo Club Bilicanas.They must know I am not a push over. Chacha died, I won't. Mtu ambaye hawezi kuheshimu mke wake aliyemzalia watoto hawezi kunyooshea mtu kidole kuhusu maadili."