BUMBULI YARIDHISHA NA SHABAHA YA SHIRIKA LA MAENDELEO (TAYODEA)

January 07, 2014
HALMASHAURI  ya  Wilaya ya Bumbuli Mkoa wa Tanga imeridhishwa na shabaha ya Shirika la Maendeleo la Vijana Mkoa wa Tanga (TAYODEA)  ya kuhamasisha vijana na kwamba limekuwa kichocheo cha maendeleo Wilayani humo.

Hayo yalielezwa na watendaji wa kata za Halmashauri hiyo  wakati wa mkutano wa wadau wa mradi wa uwajibikaji kijamii katika halmashauri ya  Bumbuli  uliyofanyika kwenye ukumbi wa Kimalube mjini Soni.

 Mkutano huo ambao pia uliwashirikisha baadhi ya wataalamu wa idara mbalimbali, walisema kuwa Tayodea  limekuwa mstali wa mbele katika kutoa elimu kwa jamii na viongozi wa ngazi zote kuhusu wajibu na haki na hivyo kuleta muamko mkubwa wa kimaendeleo.

Wamedai kuwa mbali na elimu hiyo lakini shirika hilo limekuwa mfano wa kuigwa kwa kuchangia na kushiriki katika shughuli za maendeleo ikiwemo kuibua changamoto na jinsi ya kukabiliana nazo.


Akichangia hoja katika mkutano huo, Ally Shekawa mtendaji wa Kata ya Vuga ameiifananisha Tayodea kama daraja la kuwavusha wananchi kutoka lindi la ufukara na kuingia kwenye maisha bora na yenye  matumaini kwa kuonyesha njia za kujikwamua na umasikini.

“Mimi na wenzangu tunaunga mkono juhudi za Tayodea  kuleta msukumo wa maendeleo kwa jamii kwa kusaidia miradi ya kijamii…...hili ni jambo jema na la kuigwa na wengine” alisema Shekawa.

 Naye  Nelson Pemba amepongeza juhudi za shirika hilo na kutaka kujua mikakati yake kwa upande wa kilimo ambacho ndicho tegemeo kwa wananchi waliyowengi na kwamba endapo sekta hiyo itawekewa mikakati madhubuti azma ya mabadiliko ya maendeleo itawafikia wanajamii wote.

 Pemba  ambaye  ni afisa kilimo ameshauri uongozi wa Tayodea kuangalia uwezekano wa kufadhili kilimo kama inavyofanya katika sekta nyingine ili kuiwezesha kwenda sambamba na juhudi za uzalishaji zinazoendelea kwenye maeneo mengine.

Katika mkutano huo ambao ulifunguliwa na Dk Aziz Keto kwa niaba ya Mkurugezi wa halmashuri hiyo ulihusu mashauriano ya namna y kuendesha mradi wa ufuatiliaji kijamii  kwa ushirikiano katika Kata 10  kati  ya  17 za Wilaya hiyo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »