MASHUJAA BENDI KUTUMBUIZA TANGA

January 07, 2014
Na Oscar Assenga,Tanga.
BENDI ya mziki wa Dansi nchini ya Mashujaa Music Band chini ya Rais wao Charles Baba wanatarajiwa kufanya maonyesho mawili mkoani Tanga ambapo moja litafanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Nyumbani Tanga mjini Januari 11mwaka huu.
Akizungumza na TANGA RAHA BLOG,Mratibu wa Onyesho hilo,Steven Ngonyani “Maji Marefu”alisema onyesho hilo linatarajiwa kuwa la aina yake hasa ukizingatia umahiri wa bendi hiyo mpaka ikafanikiwa chukua tuzo tano za Kilimanjaro music award hapa nchini.
Maji Marefu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) alisema kabla ya kufanyika onyesho hilo bendi hiyo itafanya onyesho lake la kwanza wilayani Korogwe Januari 10 mwaka huu ambapo watatumbuiza kwenye ukumbi wake wa Mamba Club.
  “Ninachoweza kusema maandalizi ya maonyesho yote mawili yanaendelea vizuri na ninaamini wakazi wa wilaya ya Korogwe na jiji la Tanga watapata burudani ya aina yake “Alisema Maji Marefu.
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Mashujaa Group Limited,Maximilian Luhanga alisema baada ya bendi hiyo kupata tuzo tano za Kilimanjaro Music Award wakaona wakati huu wafanya maonyesho kwa wapenzi wao ili kuweza kuwapa shukrani.
Alisema bendi hiyo baada ya kumaliza maonyesho yao mkoani Tanga itazunguka nchi nzima ili kuweza kuwapa wapenzi wao ila kitu roho inapenda kwa kuwapa burudani isiyo na kifani.
Aidha alisema wasanii wa bendi hiyo watatua mkoani Tanga wakiongoza na Rais wao Charles Baba,Rapa mahiri wao Furgeson ambaye ni pia alipata tuzo kutokana na umahiri wake.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »