Na Oscar Assenga,Tanga.
KATIBU wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa amesema
chama hicho kitahakikisha kinawapitisha wagombea wanaokubali kwenye chaguzi za
udiwani na wenyeviti wa serikali za vijiji ambao unatarajiwa kufanyika hivi
karibuni katika mikoa ya Tanga ,Kilimanjaro na Arusha kuziba nafasi zilizoachwa
wazi lengo likiwa ni kushika hatamu ya uongozi kwenye chaguzi hizo.
Golugwa
alisema hayo leo wakati akizungumza na TANGA RAHA ambapo alisema mikakati hiyo
itakwenda sambamba na ufanyaji wa kampeni za kiustarabu kwa kueleza sera makini
ambazo zitawapa hamasa wananchi kuweza kukichagua chama hicho lengo likiwa kuwapa
maendeleo pamoja na kuzipatia ufumbuzi kero zinazowakabili.
Alisema
umuhimu wa kuwaweka wagombea wanaokubali kwenye chaguzi hizo ni mkubwa sana
kutokana na kutaka kutengeza historia ya kipekee kwa kuwa na madiwani wawili
kwenye jimbo la Tanga ambao wataweza kuleta mabadiliko ya kiutendaji kwa
viongozi wengine waliopo.
“Chama chetu kitaingia kwenye mchakato wa
kuangalia nani anaweza kuipeperusha bendera kwenye chaguzi hizo na ambaye
atakuwa akikubalika kwa asilimia kubwa na wananchi wa mahala husika na sio vyenginevyo
“Alisema Bolugwa.
Alisema
kuelekea uchaguzi huo lazima wanachama na wapenzi wa chama hicho kuachana na
makundi ambayo hayana tija kwao badala yake kuwa na mshikamano ambao
utawawezesha kupata mafanikio ambayo yanapeleka kushika nyazifa za uongozi
kwenye kata na vijiji hivyo.
Uchaguzi huo
unatarajiwa kufanyika kutokana kata mbili mkoani Tanga ambazo ni Kiomoni na
Mtae Jimbo la Mlalo wilayani Lushoto viongozi wao kutokuwepo kwa kufariki na
kujiuzulu na hivyo kupelekea nafasi zao kubaki wazi.
Aliyataja
maeneo mengine yaliyowazi ambapo uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika ni kata ya
Sombeni Jimbo la Arusha,Kata ya Kiboroloni Jimbo la Moshi na Karachimbi Jimbo
la Kiteto Manyara