Magari yenye shehena ya mabomba ya maji kupitia mradi mkubwa wa marekebisho ya miundombinu ya maji kwa Mtwara mjini unaogharimu kiasi cha fedha TZS. 19 Bilioni yamepokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali ngazi ya wilaya na Chama cha Mapinduzi wakiongozwa na Mwenyekiti CCM Mkoa wa Mtwara tarehe 08/09/2023 katika kiwanja cha shule ya Msingi Lilungu.
Viongozi mbalimbali waliojitokeza wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake ya kuimarisha huduma ya Maji Mtwara mjini sambamba na Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso kwa kusimamia vema maelekezo ya Mhe Rais aliotoa juu ya kuboresha Miundombinu ya Maji Mtwara Mjini.
Aidha, akizungumza katika tukio hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mtwara (MTUWASA) Mhandisi Rejea Ng’ondya ametoa maelezo kwa mgeni rasmi Bw. Saidi Nyengedi Mwenyekiti CCM Mkoa juu ya ujio wa mabomba ya maji maboresho ya miundombinu ya maji yanayoendelea amesema dhamira ya Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha wananchi wa Mtwara wanapata huduma ya maji safi na salama na amedhamiria kumaliza kabisa changamoto ya Miundombinu chakavu Mtwara mjini ikiwa tayari Mradi wa ujenzi wa Chujio la Kusafisha Maji umekamilika na atauzindia yeye mwenyewe wiki ijayo katika ziara yake Mkoani Mtwara.
EmoticonEmoticon