Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
CCM , Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wajumbe wa mkutano
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kabla ya kufungua mkutano wao wa Tisa
uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma.
Wajumbe wa mkutano wa Umoja wa
Wanawake Tanzania (UWT) wakishangilia kabla ya ufunguzi wa mkutano huo
wa tisa wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika ukumbi wa Jakaya
Kikwete mjini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna
Mghwira akivalishwa Kitambaa kichwani mara baada ya kutangaza kuhamia
Chama cha Mapinduzi CCM katika Mkutano wa tisa wa (UWT) uliofanyika
katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira mara baada ya
kuhamia rasmi katika Chama cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa wa tisa
wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.
Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria
Nyerere akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira mara baada
ya kutangaza kuhamia Chama cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa tisa wa
UWT uliofanyika mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiimba nyimbo za CCM pamoja na
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wa pili kutoka (kushoto), Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa wa pili kutoka (kulia), Mke wa Rais Mama Janeth
Magufuli wakwanza kulia mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa tisa wa UWT
uliofanyika mjini Dodoma.
Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson akishangilia katika mkutano huo wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo mara baada ya
kufungua mkutano huo wa tisa wa (UWT) mjini Dodoma.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia wajumbe wa Mkutano wa Tisa wa UWT mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
Taifa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia Mama Maria Nyerere
ambaye pia alihudhuria katika mkutano huo wa wa Tisa wa UWT uliofanyika
mjini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akizungumza katika mkutano huo wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
Taifa CCM, Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma pamoja na bendi
ya Tanzania One Theater TOT wakati ikitumbuiza katika mkutano huo wa
tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli
akicheza pamoja na wajumbe wengine wa UWT mara baada ya ufunguzi wa
mkutano huo wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli
akizungumza jambo na Mama Maria Nyerere mara baada ya ufunguzi wa
mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT uliofanyika mjini Dodoma.
PICHA NA IKULU