Watendaji
na wataalamu wa Wilaya ya Handeni wametakiwa kusimamia na kuweka suala
la elimu ya madhara ya ukeketaji kuwa ajenda rasmi kwenye vikao vyao
ngazi ya Kata na Tarafa ili kukomesha kabisa vitendo vya ukeketaji kwa
watoto wa kike wa jamii ya wafugaji hususani pindi mradi wa “KIJANA WA
LEO” unaofadhiliwa na shirika la Amref kukoma.
.Mkuu
wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe ametoa rai hiyo leo
alipohudhuria sherehe za uvushwaji rika wa wasichana 170 wa jamii ya
wafugaji(Ndito) zilizofanyika Kata ya Malezi katika mtaa wa Kwamadule.
Mh.
Gondwe alisema kuwa ni haki ya binti anapokuwa mtu mzima na kuvushwa
rika asiweze kunyanyaswa kijinsia, kwasababu athari za ukeketaji
zinafahamika ikiwa ni pamoja na kuwa ni kitendo ambacho ni kinyume na
maagizo ya Mungu lakini pia uvunjwaji wa haki za binadamu..
Ameongeza
kuwa jamii ya wafugaji inatamaduni zilizoshiba na wanachangia kwa kiasi
kikubwa kuingizia pato na fedha za kigeni Taifa, ni utamaduni bora
unaotambulisha Tanzania kwa zaidi ya makabila 120.Watu wanapenda
tamaduni za kimasai na jamii za wafugaji wengine lakini mila ambazo ni
potofu zinazoleta maumivu katika jamii zitokomezwe.
“
sherehe na kila kitu kifanyike, watoto wafundishwe lakini ukeketaji
hapana ili tumuokoe binti huyu na maumivu makali kwa sababu morani
wamekubali kuoa wananwake ambao hawajakeketwa na kwasasa wanaoa hata
jamii zingine ambazo wanawake hawajakeketwa” alisema Mkuu wa Wilaya.
Aidha
aliwataka wataalamu wote ngazi ya Tarafa Hadi vitongoji ikiwa ni pamoja
na idara zote hususani Elimu na Mendeleo ya jamii kuendelea kutoa elimu
na kubaini wale ambao bado wanaendeleza vitendo vya ukeketaji kwa siri
ili kuchukua hatua za kisheria kwasababu wanakwenda kinyume na haki za
binadamu na kisheria hairuhusiwi.
Wakati
huohuo alizitaka jamii za kifugaji kuweka kipaumbele suala la elimu kwa
watoto kwasababu ni haki yao ya msingi na kwamba hakuna gharama yoyote
mzazi ataipata kwa kumuelimisha mtoto ili jamii yote ielimike.
Kwaupande
wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Handeni Bw.Kenneth Haule
alisema kuwa huu sio wakati wa kutegemea mifugo na ardhi katika
kuendesha maisha pekee, kwa sababu dunia na jamii kwa ujumla
inabadilika, lazima wafugaji wabadilike ili kuendana na hali ya
mazingira kwa kuwasomesha watoto wao ili waje kuelimisha jamii zao na
kupinga ukeketaji.
Meneja
mradi wa Amref Health Africa Dk.Aisha Byanaku amesema kuwa lengo kuu la
mradi ni kuborehsa afya ya uzazi kwa vijana ambao wako katika umri wa
miaka 10-24 ambapo hadi sasa elimu kwa jamii ya wafugaji imetolewa ikiwa
ni pamoja na mangariba, watoa huduma za afya na viongozi wa kimila.
Mradi
wa “KIJANA WA LEO”ulizinduliwa na Amref Health Africa Wilayani Handeni
Octoba 2015 ukifadhiliwa na Allen&Overy na big Lottery fund ambapo
hadi sasa jumla ya wasichana 830 wamefanyiwa sherehe za kimila (kuvushwa
rika) bila kukeketwa kwa Kata za Malezi,Msomera na Kwamagome za Wilaya
ya Handeni.
Sherehe
za uvushwaji rika zimehudhuriwa na wakurugenzi wa Handeni na wataalamu
mbalimbali wa Halmashauri ya Mji na Wilaya ya Handeni.
Imetolewa na:
Kitengo cha Teknolojia, Habari na Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe akikaribishwa kwenye sherehe za uvushaji rika.
Morani na Ndito wakiwa wamejipanga na kucheza wakati wa sherehe za uvushaji rika.
mangariba wakionesha namna ambavyo huwakamata wasichana (ndito) wa kimasai kuwapeleka kwenye chumba cha ukeketaji.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni akizungumza na Mangariba na kuwapongeza kuelimika kuacha vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike.
mmoja wa wazee wa kimila akishukuru nAmref kwa alimu waliyopewa juu ya
uvuhsaji rika wasichana kwa kufanya sherehe na mila zao bila kukeketa.
Mratibu wa mradi kutoka Amref Health Africa Dk.Aisha Byanaku akitoa maelezo na malengo makuu ya mradi wa KIJANA WA LEO,
mmoja wa wsichana waliovushwa rika bila kukeketwa akipokea cheti cha
kufuzu mafunzo ya kuzuia ukeketaji na mafunzo ya afya ya uzazi.