Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
NAIBU
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Ashasta Nditye, ametoa siku
14 kuhakikisha bomba la mafuta la Kimataifa linalosambaza mafuta
(TIPPER), liwe limeunganishwa kwenye mfumo unaodhibitiwa na Mamlaka ya
Bandari Tanzania (TPA) ili serikali iweze kupata mapato sahihi.
Kutokana
na bomba la tipper kuunganishwa katika bandari kumesababisha serikali
kupata mapato kwa kampuni hiyo kujisimamia yenyewe.
Akizungumza
katika ziara ya kikazi aliyoifanya bandarini hapo jana, Nditye
amesema, TPA kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na
EWURA wafanye uchunguzi wa haraka kufahamu upotevu wa mapato ya serikali
yaliyotokana na Tipper kujiunganishia mafuta kutoka kwenye meli bila
kupitia katika kituo cha Kurasini Oil Jet (KOJ).
Amesema
Tipper wamekiuka maagizo ya Waziri Mkuu, Kassim Majaaliwa yaliyolewa
Februari mwaka jana ya kutaka waunganishe bomba lao katika mfumo wa TPA
ili kufahamu kiwango cha mafuta wanayoyachukua.
"
Wizi wa waziwazi tangu Februari mwaka jana alipoagiza Waziri Mkuu
hadi leo TIPPER mmeshindwa kuunganisha bomba lenu hali inayochangia
mapato ya Serikali kuzidi kupotea," alisema Nditye.
Amesema
TIPPER waliagizwa na waziri ndani ya mwezi.mmoja wawe wamejiunga
katika.mfumo huo lakini cha ajabu maaagizo yamekiukwa hali inayoashiria
bado kuna ujanja unaendelea.
Amesema
haiwezekani TIPPER wakajiunganisha wenyewe halafu wakajisimamia
wao.kufahamu kiwango cha mafuta ya dizeli na ya kula wanayotumia.
Aliagiza pia TPA iimarishe ulinzi kwa mtoa taarifa za upotevu wa mafuta hayo na endapo atapata madhara Serikali.itachukua hatua.
Awali
Meneja Mafuta wa Bandari ya Dar es Salaam, Kapteni Paul Paul alisema
TIPPER wamekiuka.agizo la waziri Majaliwa ambapo hadi sasa
hawajajiunganisha katika mfumo wa bomba linalodhibitiwa na TPA.
Amesema
hadi sasa makampuni yaliyounganishwa katika mfumo wa TPA ili kuangalia
kiasi cha mafuta kinachotumika ni pamoja na Lake Oil, Moil, Hass pamoja
na World Oli/Sahara/Kobil.
Paul alisema kitendo cha mita za mafuta ya TIPPER kudhibitiwa na wenyewe linatakiwa liangaliwe kwani lina athari.
Mkurugenzi
Msaidizi wa TIPPER, Paul Mzava alisema, walipokea.maelekezo kutoka kwa
Msajili wa hazina kusitisha kuhamishwa kwa bomba hilo mara baada ya
waziri Majaaliwa kutoa agizo. Alisema taarifa hizo walizipeleka kwa
uongozi wa TPA kwa maandishi.
Mzava
alisema kuhamishwa kwa bomba linalomilikiwa na TIPPER kulipeleka kwenye
mfumo wa TPA kuna umbali wa mita 400 hivyo waliona ni gharama
kulihamisha. Alisema pia waliona katika kituo kile cha KOJ kitahamishwa
muda wowote hali itakayochangia hasara.
Akijibu hoja hizo, Mhandisi Deusdetit Kakoko alisema alichokuwa anafahamu ni kuwa tayari TIPPER wamejiunga na mfumo wao.
"Binafsi
nilipewa taarifa kuwa tayari TIPPER wamejiunga katika mfumo wetu
kinyume na hapo sina taarifa nyingine,"alisema Kakoko.
Alisema
kutokana na hali hiyo atahakikisha anafuatilia undani jambo hilo pamoja
na.kuwawajibisha watendaji waliokwenda.kinyume na agizo hilo.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano,
Mhandisi Ashasta Nditye akizungumza na Menejimenti ya Mamlaka ya
Usimamizi wa Bandari (TPA) katika ziara yake alipotembelea mamlaka hiyo
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA),
Mhandisi Deusdedit Kakoko akitoa taarifa za utendaji wa mamlaka hiyo
kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Ashasta Nditiye (Kushoto) wakati Naibu Waziri
huyo alipotembelea mamlaka ya Bandari jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano,
Mhandisi Ashasta Nditiye akizungumza katika ujenzi wa scanner ya
ukaguzi katika bandari ya Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano
,Mhandisi Ashasta Nditiye akifanya majumuisho baada ya kufanya ziara
katika bandari ya Dar es Salaam.