“HITILAFU YA UMEME YAUNGUZA BAADHI YA VIFAA OFISI YA ELIMU SEKONDARI JIJI LA TANGA”

December 08, 2017
Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji mkoa
wa Tanga,Inspekta Kumenya Bakari akizungmza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Jiji wakitoa
vitu nje kwenye ofisi ya Elimu Sekondari ya Jiji hilo baada ya kuungua kutokana na hitilafu ya umeme .

HITILAFU ya Umeme iliyotokana na mgandamo wa hewa imesababisha ofisi ya Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Jiji la Tanga kuungua moto ikiwemo baadhi ya vitu vilivyo kuwemo ndani kabla kuzimwa ili usiweze kusambaa kwenye maeneo mengine ndani ya Halmashauri ambao ungeweza
kuleta athari kubwa.

Jitihada za kuufanya moto huo usiweze kusambaa kwenye maeneo mengineulifanywa na watumishi wa halmashauri hiyo  ambao walitumia vifaa vya kuzimia moto huo baada ya kupatiwa elimu ya kupambana na majanga ya
moto.

Akizungumza jana,Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Tanga,Inspekta Kumenya Bakari alithibitisha kuungua kwa ofisi hiyo ambapo alisema tukio hilo lilitokea  Desemba  8 asubuhi  saa tano asubuhi baada ya kupata taarifa kutoka kwa kijana wa boda boda na ndipo walipoamua
kutoka na magari yao.

Alisema pamoja na kupewa taariufa hizo wakiwa wanajiandaa kufika eneo la tukio wakasikia alamu iliyopo ofisini iliwaonyesha kuna moto unawaka eneo la ofisi ya halmashauri na ndipo vijana wakatoka kwa haraka sana pamoja na askari waende kuona na kuchukua hatua ya kuuzima.

Aidha alisema ushupavu wa watumishi hao kuwahi na kuuzima moto huo kwa kuanzia na uzimaji wa swichi kubwa ya umeme inatokana na elimu ambayo walikwisha kuwapatia namna ya kukabiliana na majanga ya namna hiyo pindi yanapotokea kwenye maeneo yao na hivyo kuweza kuuzima mapema.

Naye kwa upande wake,Msaidizi wa Afisa Habari wa Kikosi hicho mkoani Tanga,Sajenti Mussa Msengi alisema baadhi ya vitu ambavyo vimeungua niSimu moja,pazia, Fax  Mashine,Printer,Meza ,Rimu na Nyaraka mbalimbali
zilizokuwemo ndani ya ofisi hiyo.

Akizungumzia tukio hilo, Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Alhaj
Mustapha Selebosi alisema baada ya kutokea tukio hilo watakachokifanya hivi sasa ni kurekebisha kutokana na kuwepo kwa vitu vingi ambavyo vimejaa hivyo kunaweza kupelekea matukio ya namna hiyo.

Alisema iwapo wasingekuwa na mitambo yao ya kuzimia moto inaweza kupelekea hasara kubwa kwa kuungua jengo lote.

“Kwanza nishukuru kuwepo kwa mitambo yetu wenyewe ya kuzimia moto hasa yanapojitokeza majanga ya moto ni moja kati ya vitu muhimu vilivyosaidia kukabiliana na janga hili “Alisema.

MBUNGE WA TANGA ASHIRIKI KUUZIMA MOTO.

Awali akizungumza na gazeti hili,Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) AlhajiMussa Mbaruku  alikuwa ni miongoni mwa  watu walioshiriki kwenye zoezi la kuuzima moto huo ili usiweze kuleta madhara katika maeneo megine.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa tukio hilo,Mbunge Mussa alisema ipo haja halmashauri kuongezwe vifaa vya kuzimia moto lakini pia kuwepo na alama ambazo zitakuwa zikitoa ishara wakati yanapojitokeza mambo ya namna hiyo.

"Kwa kweli hali ilikuwa mbaya sana wakati wa tukio hili linatokea kwa sababu na mimi nilikuwepo na nimeshuhudia lakini niseme upo umuhimu mkubwa kuwepo kwa vifaa vya kutosha vya kuzimia moto katika maeneo mbalimbali ya majengo ya serikali kuweza kunusuru na hasara zinazoweza kutokea kama ilivyokuwa leo(jana) tulivyoweza kupambana na moto na
kuuzima "Alisema.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »