Waziri
wa kazi, ajira, sera, bunge, vijana na wenye ulemavu Mhe. Jenista
Mhagama amelipongeza Shirika la NSSF kwa kuwa mfano wa kuigwa katika
nyanja za kiuchumi na kijamii. Waziri mkuu aliyasema hayo katika mkutano
wa wadau wa NSSF unaoendelea katika Kituo cha kimataifa cha mikutano
AICC, Arusha
Waziri
wa kazi pia alipongeza NSSF kwa kuandaa mkutano wa wadau unaofanyika
hapa jijini Arusha, alisema mkutano huo siyo muhimu kwa NSSF na wadau tu
bali pia kwa maendeleo na ustawi wa Taifa letu. Pia alifurahi kupata
nafasi ya kufuatilia utendaji wa NSSF pamoja na kuona moja kwa moja
kutoka kwa wadau wa NSSF.
Pia
aliwapongeza wadau wa NSSF kwa kuitikia wito wake wa kuja kushiriki
ili kupata taarifa za utekelezaji wa maazimio waliyokubaliana mwaka
jana, taarifa za utendaji na kuchangia mawazo yatakayoleta tija ya
kulijenga Shirika. Aidha, aliwapongeza Wageni mbalimbali katika mkutano
huo ambao ni pamoja na Mhe. Anthony Mavunde, Katibu Mkuu Ndg. Eric
Shitindi, Mkurugenzi Mkuu wa SSRA na Wakurugenzi wa Mifuko mingine ya
Pensheni.
Vile
vile Waziri wa kazi alitoa pongezi kubwa kwa namna ambavyo NSSF
ilivyojitolea katika kutekeleza jukumu la kukuza Uchumi wa Viwanda
kwani alisema Ujenzi wa Taifa si jukumu la Serikali Kuu peke yake bali
ni la kila Mtanzania mmoja mmoja, taasisi na makampuni, na ndio maana
NSSF pamoja na kuwa na jukumu la hifadhi ya jamii kwa mujibu ya sheria
yake husika, imeona haja ya kupanua wigo wa uwekezaji wake na kuelekea
katika viwanda jambo ambalo litaongeza ajira, kuongeza uzalishaji, na
kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.
Waziri
Mhagama alitoa mfano katika uwekezaji wa NSSF katika kukuza viwanda
tumeshuhudia uwezekano wa kuzalisha ajira za moja kwa moja kwa
Watanzania kutoka na uwekezaji ilioufanya katika viwanda mbali mbali.
Nichukue fursa hii kuipongeza NSSF kwa kutoa mkopo wa shilingi bilioni
3.1 kwa lengo la kuongeza uzalishaji katika kiwanda cha madawa kilichopo
Kibaha chini ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC). Katika kiwanda
hiki ambapo ajira 100 zimezalishwa. Uzalishaji wa viuadudu ulianza Mwezi
Desemba 2016 na mpaka sasa kiwanda kimezalisha jumla ya lita 327,400
ambazo ziliuzwa katika masoko ya ndani na nje.
Shirika
lilitoa Mkopo kwa ajili ya upanuzi wa Kiwanda cha Chaki kilicho chini
ya Usimamizi wa Halmashauri ya Maswa, Mkoani Simiyu mnamo mwezi June,
2017. Mkopo huu kwa ujumla utaongeza uzalishaji wa chaki kutokea vipande
432,000 vya chaki nyeupe (sawa na Katoni 180) kwa siku hadi vipande
milioni 4.8 vya chaki nyeupe na za rangi (sawa na Katoni 2,000) kwa
siku. Ongezeko la uzalishaji huu wa chaki utasaidia kuendeleza Sera ya
Serikali ya “Elimu Bila Malipo” kwani itasaidia kupunguza mahitaji
makubwa ya chaki katika shule za awali na msingi. Jumla ya Ajira 100 za
moja kwa moja zinatarajiwa kutokana na uwekezaji huu.
Pia
aliwapongeza NSSF kwa kushirikiana na PPF, na Jeshi la Magereza kupitia
Kampuni ya Mkulazi, wamewekeza katika Mradi mkubwa wa shamba la miwa na
Kiwanda cha Sukari kilichopo Mbigiri ambapo tayari hatua za upandaji
miwa zimeanza nami nikiwa miongoni mwa j waliopata fursa ya kupanda miwa
yamwanzo kabisa.
Kiwanda hiki Cha Mbigiri kitakapokamilika kinatarajiwa kuzalisha tani 50,000 za sukari kwa mwaka. Mpaka sasa mradi huu umezalisha ajira 300 za moja kwa moja na pia kupitia mpango wake wa wakulima wa nje katika eneo la Dakawa, imeweza kuandikisha jumla ya wakulima 1,500 wanaotegemewa kuanza kilimo cha miwa kuanzia mwezi Novemba, 2017 ambao watalima heka 15,297.
Kiwanda hiki Cha Mbigiri kitakapokamilika kinatarajiwa kuzalisha tani 50,000 za sukari kwa mwaka. Mpaka sasa mradi huu umezalisha ajira 300 za moja kwa moja na pia kupitia mpango wake wa wakulima wa nje katika eneo la Dakawa, imeweza kuandikisha jumla ya wakulima 1,500 wanaotegemewa kuanza kilimo cha miwa kuanzia mwezi Novemba, 2017 ambao watalima heka 15,297.
Hapo
nyuma maeneo haya yatakayolima miwa na wakulima wa nje ama hayakuwa
yakilimwa kitu chochote kama mashamba pori au yalikuwa yakilima mazao
yasiyo na tija kama itakavyokuwa kwa zao la miwa. Hii ni hatua kubwa na
ya kupongezwa sana Pia NSSF na PPF kupitia Mkulazi, watajenga Kiwanda
cha Sukari kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha tani 200,000 kwa mwaka,
kiwanda hicho kitajengwa katika eneo la Mkulazi lililopo Ngerengere,
Mkoani Morogoro, ambapo kinamtazamo wa kutoa ajira zaidi 100,000 kwa
watanzania.
Alisema
Mbali na kuzalisha ajira hizo, NSSF kupitia miradi inayoifadhili ya
kufufua viwanda vya iliyokuwa National Milling Corporation (NMC) ambavyo
kwa sasa vipo chini ya Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB)
inategemewa kuwa itakapokamilika itazalisha jumla ya ajira 30,000.
Kiwanda kilichopo Kizota, Dodoma kina uwezo wa kuzalisha tani 60 za unga
na tani 20 za mafuta ya alizeti. Kiwanda hiki kitatoa ajira 6000 za
moja kwa moja, na kiwanda cha NMC Mwanza chenye uwezo wa kuzalisha tani
250 za unga na tani 60 za mchele kinatarajiwa kutoa ajira za moja kwa
moja 24,000.
Na
alihitimisha kwa kusema Kwa uwekezaji huu, maana yake ni kwamba mifuko
hii itaondoa tatizo la ajira katika nchi, itasaidia kuweka ushindani
katika soko na hivyo kushusha makali ya bei katika bidhaa zitakazokuwa
zikizalishwa na pia itasaidia serikali kukusanya kodi na hivyo kuisaidia
kuwekeza katika miradi mingine ya kimaendeleo na kijamii. Mbali na
haya, Mifuko hii itapata wanachama wapya na kukusanya michango zaidi na
kuwekeza zaidi ili kuweza kutimiza malengo yake ya msingi ya Hifadhi ya
Jamii. Hivyo, hatuna budi kwa pamoja kutoa pongezi za dhati kwa ubunifu
mkubwa unaonyeshwa na mifuko hii
Nae
Mkurugenzi mkuu wa NSSF Prof Godius Kahyarara alisema Kwa muda mfupi,
Mfuko wa NSSF umeonyesha ufanisi mkubwa na mafanikio ya kuridhisha kwa
kutunisha mapato yake kwa kuongeza ukusanyaji wa michango, kupunguza
matumizi ya uendeshaji wa shughuli zake na pia kuongeza wigo wa
uwekezaji kwa kipindi kifupi cha uwekezaji kutoka Shilingo Bilioni 12
mwezi Aprili mwaka 2016 hadi Shilingi Bilioni 418.82 mwezi Juni mwaka
huu, 2017. Mfuko pia umeweza kupunguza malipo hewa ya kujitoa kwa
asilimia 127 na hivyo kuokoa kiasi cha Shilingi Bilioni 160 kwa kipindi
cha mwaka mmoja. Taarifa za uwezo wa fedha zinaonyesha kuwa tumeweza
kuwekeza takribani Shilingi bilioni 50 za Tanzania kupitia hisa za
Vodacom zilizowekwa sokoni mwaka huu. Zaidi ya hapo, tumeweza pia kulipa
malimbikizo yote ya kodi kwa zaidi ya Shilingi bilioni 94 za Tanzania
na pia kumaliza malipo yote ya mikatabayenye thamani ya Shilingi 169.5
bilioni za Tanzania.
Mkutano
huu wa Wadau wa Mfuko wa NSSF unafanyika katika kipindi ambacho
Serikali ya Awamu ya Tano imeweka mikakati na malengo muhimu ya
mabadiliko ya kukuza uchumi wa viwanda. NSSF imawahakikishia ushiriki
wake katika kutekeleza Sera ya Serikali ya kukuza na kujenga uchumi wa
viwanda. Mfuko wa NSSF umejikita katika kukuza uchumi kupitia Sekta ya
Viwanda kabla ya miaka ya 1990 wakati ambao Tanzania ilijikita katika
mapinduzi ya uchumi wa viwanda. Mifano michache ni ushiriki wa Mfuko wa
NSSF katika uwekezaji wa ubia na viwanda vya Aluminum Africa, Kwanza
Bottles, Phantom Limited, Mbeya Cement, Meditech, General Tyre, Katani
Limited, Kagera Sugar, Tanzania Pharmaceuticals Limited, 21st Century
na Dar Cement Company.
Kupitia
uzoefu mpana tuliopata katika ushiriki wa maendeleo ya viwanda, Mfuko
wa NSSF upo tayari kuongeza juhudi za kusaidia malengo ya Mheshimiwa
Rais John Pombe Magufuli ya kujenga “Tanzania ya Viwanda”.Alisema,
Wakati huu tunapotekeleza azma yetu ya kusaidia juhudi za Serikali
kujenga uchumi wa viwanda, Mfuko wa NSSF unaendelea kutekeleza mikakati
yake ya shirika kuwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Unoongoza miongoni mwa
Mifuko yote Barani Afrika ifikapo mwaka 2020. Ili kufikia lengo hilo,
Mfuko unahitaji wanachama 1,823,927 na makusanyo ya michango kiasi cha
Shilingi Trilioni 1.76 za Tanzania kila mwaka.
Alisema
Mfuko wa NSSF umetumia kiasi cha Shilingi za Tanzania17,384,771,999 kwa
kutoa huduma za Bima ya Mafao ya Afya. Mafao kwa Bima ya Afya ni
muhimu ambao wanachama 443,293 walipewa huduma hizo. Mfuko pia
umewafikia wanachama 121,460 kutoka Sekta isiyo Rasmi kwa kuandikisha
wanachama kutoka makundi ya wajasiriamali wadogo wakiwemo Wachimbaji
wadogo wadogo wa Madini, Wavuvi, Waendesha Pikipiki (Boda Boda),
Wachuuzi wadogo wadogo wa bidhaa (Machinga), Mama Lishe pamoja na
Wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini
Vile
vile Prof Kahyarara alisema Kuhusu ushiriki wa Mfuko wa NSSF katika
kusaidia na kuwajibika kwa Jamii ya Wanzania, Mfuko wa NSSF umesaidia
makundi kadhaa ya wanachi kwa kutoa na kuboresha huduma za Afya kwa
kujenga Vituo vya Afya, Zahanati, kusaidia utoaji wa huduma za afya na
pia kampeni ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza. Michango mingine ya
Mfuko pia imelenga kusaidia kampeni za kupambana na Maambukizi ya
Virusi vinavyoeneza Ukimwi kupitia TACAIDS katika Mpango wa Miaka Mitano
wa kupambana na kuenea kwa Virusi vya VVU.
Mfuko
wa NSSF pia umesaidia ununuzi wa Madawati katika Shule kadhaa za
Tanzania ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Mh. Rais John Magufuli ya
kupanua elimu nchini Tanzania. Mfuko pia umesaidia kukarabati madarasa
na maabara kadhaa ya shule nchini. Mfuko wa NSSF pia umesaidia maeneo
ya usalama kwa njia ya michango kwa kujenga Kituo cha Polisi cha Kiluvya
pamoja na Nyumba za Askari Polisi, pia Wiki ya Nenda kwa Usalama
Barabarani. Pamoja na misaada mingine, Mfuko wa NSSF umesaidia kuchangia
katika maafa yaliyoikumba Tanzania ikiwemo Majanga ya Asili na Moto.
Mfuko umechangia kujenga upya miundombinu iliyoharibiwa na mafuriko huko
Lindi, Nasibugani, Mtwara na Shule ya Sekondari ya Moreto.
Shule
kadhaa zilizoharibiwa pamoja na mabweni na madarasa yake kubomolewa
kutokana na Tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera pamoja na wahanga wa
Tetemeko hilo walipatiwa misaada mbalimbali. Mfuko wa NSSF pia umetoa
msaada kwa wakazi wa Kagera kununua mbegu za viazi vitamu vinavyoota na
kukomaa haraka wakati wa uhaba wa mvua kutokana na mashamba mengi ya
nafaka kuharibiwa na Tetemeko hilo mwaka jana.
EmoticonEmoticon