Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe January
Makamba akifafanua jambo mbele ya
kusanyiko la wanajumuiya ya Wafanyabiashara wa Zanzibar (hawapo pichani).
Kikao hicho kimefanyika hii leo eneo la Kinazini Zanzibar. Wengine katika picha
ni viongozi wa Jumuiya hiyo.
Sehemu ya wafanyabiashara wa
Zanzibar wanaounda Jumuiya ya Wafanya Biashara wa Zanzibar wakiwa katika kikao
na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mhe January Makamba aliyewaalika kujumuika kubadilishana
uzoefu na kuwaomba waainishe changamoto
zinazowakabili na kuona namna bora ya kuzipatia ufumbuzi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe January
Makamba akisalimiana na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais -
Muungano katika Serikali ya awamu ya nne Mhe. Mohammed Seif Khatibu ambaye pia
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Zanzibar Media Coorporation, Waziri Makamba alipata
pia wasaa wa kufanya mahojiano katika chombo cha Habari cha Zenji FM na Zenji
TV
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe January
Makamba akifanya mahojiano maalumu katika Kituo cha Redio cha Cocunut FM
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe January
Makamba ameanza ziara ya kikazi ya siku saba visiwani Zanzibar. Katika siku ya
kwanza Mhe. Makamba amepata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Jumuiya
ya Wafanyabiashara wa Zanzibar kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kubaini fursa
na changamoto zinazowakabili na kuona namna bora ya kupata ufumbuzi.
Miongoni mwa changamoto
zilizojadiliwa na kuwekewa mikakati ya utekelezaji ni pamoja na masuala ya
kodi, namna ya kunufaika kutoka na fursa zilizopo baina ya pande zote mbili za
Muungano na kuondoa vikwazo vinavyotokana na changamoto hizo ili kuleta
ufanisi.
Mhe. Makamba amewahakikishia wana
juimuiya hao kuwa Ofisi yake itaratibu vikao kati ya Ofisi yake na
wafanyabiashara hao ili kupata fursa ya kutoa mrejesho wa utekelezaji wa mambo
waliyokubaliana.
Mbali ya kukutana na wafanyabiashara
hao Waziri Makamba pia amepata fursa ya kutembelea Vyombo mbalimbali vya Habari
hapa Unguja kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya Muungano. Vyombo
vilivyotembelewa ni pamoja na Zenji FM na Zenji Tv, Bahari FM na Cocunut FM.
Ziara ya Waziri Makamba katika siku
pili atatembelea Miradi mikubwa ya Mazingira na kuwa na Vikao na Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRB).
EmoticonEmoticon