Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiongea na wanafunzi,wazazi na walimu wakati wa mahafali ya kidato cha nne mwaka huu 2017 katika shule ya sekondari ya Kwakilosa iliyopo katika manispaa ya Iringa
Baadhi ya wanafunzi na wazazi walihudhuria sherehe za kuhitimu kwa wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Kwakilosa iliyopo kata ya Mwangata.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akimkabidhi cheti mmoja ya wanafunzi wa kike aliyehitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Kwakilosa
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mbunge
wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati
amekerwa na uwepo wa mimba za utotoni katika shule ya sekondari ya Kwakilosa
iliyopo kata ya Mwangata manispaa ya Iringa kwa kuwa kitendo hicho
kinachosababisha kushuka kwa elimu katika shule hii.
Akizungumza
wakati wa shererhe za kuhitimu elimu ya sekondari kwa wanafunzi wa kidato cha
nne mwaka huu Kabati alisema kuwa amesikitishwa kusikia kila mwaka kuna
wanafunzi wanakatisha masomo kwa ajili ya kupata ujauzito.
“Jamani
tumekuwa tukitoa elimu kila mara juu ya madhara yanayotoka na upatikanaji wa
mimba za utoto za hiii shule imekuaje kila mwaka wanafunzi wanapata mimba hii
haikubariki katika jamii kabisa maana hawa wanafunzi ndio tegemeo la taifa kwa
sasa” alisema Kabati
Kabati
aliwataka wazazi na walimu kuwalinda wanafunzi wa kike ili wasikumbane na ardha
ya kupata mimba wakiwa watoto wadogo kwani kunapoteza muelekeo wa maisha yao na
maendeleo ya taifa kwa ujumla.
“Haiwezekani
kila mara wazazi mnakuwa wa kwanza kuwa chanzo cha kuwaharibu watoto na kwanini
wazazi mnafanya hivyo maana watoto hawa ndio watakao wasaidia hapo baadae ndio
maana mkiwa mmezeeka kwa hiyo ndio watakuwa msaada katika maisha yenu naombeni
muwatunze watoto wenu” alisema Kabati
Aidha
Kabati aliwataka wanafunzi wote mkoani Iringa na Tanzania kwa ujumla kuacha
kufanya mapenzi wakiwa na umri kama wao hivyo wanapaswa kujilinda ili kufikia
malengo yao waliojiwekea na walidhike na kipato walicho nacho wazazi wao.
“Hivi
kaka mimi ningeanza mapenzi nikiwa na umri kama wenu unafikiri ningefikia
malengo haya niliyonayo hivyo nawaomba msifanye mapenzi mkiwa na umri mdogo ili
baadae mje kufikia malengo yenu” alisema Kabati
Kwa
upande wake mkuu wa shule hiyo Hudson Luhwago aliwatupia lawama wazazi na
walezi wa wanafunzi wa shule hiyo kwa kutowalea katika malezi mazuri wanafunzi
hao.
“Yaani
kabisa mzazi anakuja na wanafunzi anamuombea ruhusa kuwa walikuwa fiesta wote
hivyo mtoto amechoka hawezi kuja shule hii ni aibu na ukweli unaoendelea kwa
baadhi ya wazazi wa wanafunzi wa shule hii” alisema Luhwago
Luhwago alisema kuwa kuna baadhi ya wanafunzi
wanawanaume zaidi ya watano na wazazi wanayajua hayo lakini wanashindwa
kuwakemea watoto wao na ndio maana wanakuja shule wakiwa na kiburi hata kwa
walimu.
“Wanafunzi
hawa wanaomaliza hitimu shule leo walikuwa wanakiburi kwa sisi walimu hadi
ikabidi tukae kama wanalimu tuwajadili lakini chanzo chote ni malenzi mabaya
wanayoyapata kutoka kwa baadhi ya wazazi au walezi wao” alisema Luhwago
Akisoma
risala kwa mgeni rasmi makamu mkuu wa shule Praygod Makongwa alisema kuwa hadi
sasa kuna mwanafunzi ameachishwa shule akiwa kidato cha kwanza kwa sasbabu ya
kuwa mujamzito na hata hawa wanaohitimu hii leo mwenzao mmoja alikatisha masomo
akiwa kidato cha pili kwa kuwa na ujauzito.
“Sisi
kama walimu wa shule hii tushazoe kuona wanafunzi wanakatisha masomo kwa ajili
ya kupata mimba na ukiangalia kwa umakini walimu tunawalea wanafunzi kwa
maadili yanayotakiwa tatizo lipo kwa wazazi hao unakuta mtoto na mzazi wapo
disco pamoja wanakunywa pombe pamoja sasa hapo utapata matokeo gani?” alisema
Makongwa
Lakini
Makongwa alisema kuwa shule imejiwekea mikakati ya kuhakikisha inajenga majengo
ya mabweni kwa wanafunzi ili kumaliza tatizo la mimba za utoto na kuboresha
elimu ya shule ya sekondari ya Kwakilosa.
EmoticonEmoticon