Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba (kushoto) akimsikiliza
Kapteni Abdallah Juma Abdallah Mkurugenzi Mkuu wa Bandari – Zanzibar
alipokuwa akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa kazi za bandari mara
baada ya Waziri Makamba kupata fursa ya kuwatembelea.
Viongozi waandamizi wa Bandari –
Zanzibar wakifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mhe January Makamba alipotembelea bandari hiyo
hii leo kujionea utendaji kazi wao na kuwapa fursa ya kuianisha
changamoto zinazowakabili na kuweka mikakati ya kukabiliana nazo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba (katikati) akifafanua
jambo kwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar wa (pili kulia).
Waziri Makamba amefanya ziara ya kutembelea ofisi zao na kupata fursa
ya kufanya majadiliano kwa manufaa na ustawi wa Muungano wetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba akiwa katika kikao na
Menejimenti ya Bodi ya Mapato Zanzibar. Wa pili kushoto ni Kamishna wa
Bodi Bw. Amour Hamil Bakari na Bi. Khadija Shamte Naibu Kamishna.
Waziri Makamba yuko ziarani Zanzibar kutembelea Taasisi za Muungano na
zile zisizo za Muungano.
…………………………………………………………………….
Imebainika kuwa Bandari ya
Zanzibar ni miongoni mwa Vyanzo vya Mapato vinavyopelekea ukuaji wa
uchumi baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kutokana na fursa zilizopo katika nyanza za
biashara.
Hayo yamebainishwa leo na
Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Zanzibar Captain Abdallah Juma Abdallah
katika siku ya pili ya ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ambapo amepata fursa ya
kutembelea Bandari ya Zanzibar.
Katika siku ya pili ya ziara yake
ya siku saba Visiwani Zanzibar Waziri Makamba amebainisha kuwa lengo la
ziara yake ni pamoja na kufuatilia utekelezaji wa masuala
waliyokubaliana katika vikao baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar katika vikao vya mashirikiano.
“Niko Zanzibar kwa ziara ya
kikazi na nimejikita zaidi katika kushughukikia masuala ya uchumi ikiwa
ni pamoja na masuala ya Bandari, Forodha, Kodi na kubaini changamoto
zilipo, utekezaji wa maazimio yaliyokubaliwa katika vikao vya
majadiliano na kuangalia maeneo mapya yanayohitaji kuingizwa katika
mfumo wa utatuzi,” Makamba alisisitiza.
Waziri Makamba amesema kuwa
kuwepo kwa bandari ni ufanisi kwa uchumi na ni namna bora ya kuimarisha
Muungano na ustawi wa Zanzibar na pande zote mbili za Muungano hazina
budi kuondoa changamoto zilizopo kwa manufaa ya wote.
Waziri Makamba pia amepata fursa
ya kutembelea Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Mapato Zanzibar na
kuwafahamisha kuwa lengo la Serikali zote mbili ni kuhakikisha kuwa
pande zote mbili za Muungano zinanufaika na fursa za uchumi zilizopo, na
kila upande unufaike na fursa zilizopo katika mambo ya Muungano na yale
yasiyo ya Muungano.
Katika ziara hiyo Waziri Makamba
amewataka watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania upande wa Zanzibar
kuzifanyia kazi changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza kwa haraka,
kupunguza urasimu na kuongeza elimu kwa umma ili kujenga uelewa kwa
wananchi juu ya mambo yanayopaswa kuzingatiwa na yale yasiyopasa ili
kuondoa vikwazo vinavyojitokeza katika bandari ili kuondoa malalamiko ya
wananchi.
Nae Naibu Kamishna wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania kwa upande wa Zanzibar Bw. Mcha Hassan Mcha amesema
kuwa ni vema wananchi wazingitae kanuni, taratibu na miongozo iliyopo
ikiwa pamoja na kupata risiti halali kwa kila bidhaa wanazonunua ili
kuepuka usumbufu pindi wasafirishapo bidhaa baina ya Tanzania bara na
Zanzibar.
Ziara ya Waziri Makamba visiwani Zanzibar itaendelea kesho kwa kutembelea miradi mbalimbali ya Mazingira.
EmoticonEmoticon