Mtendaji
Mkuu wa Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bw. Charles
Senkondo akieleza kuhusu utendaji wa taasisi anayoiongoza wakati wa
ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb)
aliyoifanya mapema leo jijini Dar es Salaam.
Afisa
kutoka Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) akiwasilisha mada
kuhusu kazi na mafanikio ya wakala wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) katika wakala hiyo mapema
leo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akifuatilia mada
iliyowasilishwa kuhusu kazi na mafanikio ya TaGLA alipofanya ziara ya
kikazi katika Wakala hiyo mapema leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake
ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Bi. Susan
P. Mlawi, na Kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu wa TaGLA, Bw. Charles
Senkondo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akisisitiza jambo wakati
akizungumza na Watumishi wa TaGLA mapema leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akipata maelezo kuhusu
mifumo ya TEHAMA inavyofanya kazi wakati wa mikutano ya kieletroniki
(Video Conference) katika ofisi za TaGLA wakati wa ziara ya kikazi
aliyoifanya mapema leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akipokea taarifa (nakala
ngumu na laini) zenye shughuli zinazofanywa na Wakala ya Mafunzo kwa
Njia ya Mtandao (TaGLA) kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo, Bw.
Charles Senkondo baada ya kumaliza ziara ya kikazi katika wakala hiyo
mapema leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akipokewa na watumishi wa
Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma alipofanya ziara
ya kikazi katika Bodi hiyo mapema leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu
ya watumishi wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma
wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakati
wa kikao kazi katika ofisi za Bodi hiyo mapema leo jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bw. Donald
Ndagula akitoa neno la shukurani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu)
Mhe. George H. Mkuchika (Mb) mara baada ya Waziri kumaliza kuzungumza na
watumishi wa bodi.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Kapt. (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akijionea utunzaji wa
kumbukumbu alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi ya Idara ya
Kumbumbuku na Nyaraka za Taifa leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akipokea nyaraka mbalimbali
zinazohusu utunzaji wa kumbukumbu kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara
ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Charles Magaya katika ofisi za
Idara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
Bodi
ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma imeagizwa kufanya
utafiti wa kina utakaowezesha kuwa na uwiano sawa wa malipo ya mishahara
na masilahi ya watumishi wote serikalini.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Kapteni (Mstaafu), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) amesema hayo leo wakati
wa ziara ya kikazi katika Ofisi za Bodi ya Mishahara na Masilahi katika
Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam.
Mhe.
Mkuchika amesema kuna baadhi ya taasisi/Idara za Serikali zinalipa
watumishi wake mishahara mikubwa tofauti na taasisi nyingine jambo
ambalo limekuwa likisababisha watumishi kutotulia sehemu moja na
kutafuta masilahi bora zaidi sehemu nyingine.
“Hii
haiwezekani, mmesoma darasa moja, fani moja na mko cheo kimoja, lakini
mnalipwa mishahara tofauti wakati serikali ni moja, ni lazima mlifanyie
utafiti wa kina suala hili. Masilahi ya watumishi wa umma lazima yawe
sawa” Waziri
Mkuchika
amesisitiza na kuongeza kuwa kumekuwa na malalamiko mengi serikalini
kuhusu tofauti kubwa ya mishahara miongoni mwa watumishi wa Serikali Kuu
na baadhi ya taasisi za serikali.
Aidha,
Mhe. Mkuchika amewataka watumishi wa Bodi hiyo kuwa wabunifu na
kupendekeza mambo ambayo yatawavutia Watumishi wa Umma kufanya kazi
Serikalini kwa dhati kwa kuzingatia taaluma zao na mgawanyo wa majukumu.
“ Kila mtumishi ana taaluma yake na mgawanyo wa majukumu aliyopewa
wakati anaanza kazi, hivyo ni vema kila mtu akazingatia hayo ili kuwa na
utendaji bora serikalini,” Mhe. Mkuchika amesema.
Mhe.
Mkuchika, ameendelea na ziara ya kikazi ya kujitambulisha na kujifunza
kazi mbalimbali zinazofanywa na taasisi zilizo chini ya ofisi yake,
ambapo leo ametembelea Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA),
Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma na Idara ya
Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa.
Bodi
ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma ni matokeo ya Tume ya
Rais ya Malipo ya Mishahara ya mwaka 2006 iliyopewa jukumu la kuishauri
Serikali namna ya kuboresha malipo ya mishahara na motisha nyingine
katika Utumishi wa Umma.
EmoticonEmoticon