Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh.
Dkt.Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman
Dkt. Mohamed Hamad Al Rumhy alipokuwa akiwasili kwenye tukio la Ngoma
na nyimbo za Taifa la Oman, Jijini Dar es salaam jana Oktoba 18, 2017
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh.
Dkt.Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe.
Salem Ben Nasser Al Ismaily, Kulia ni Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman
Dkt. Mohamed Hamad Al Rumhy alipokuwa akiwasili kwenye tukio la Ngoma na
nyimbo za Taifa la Oman, Jijini Dar es salaam jana Oktoba 18, 2017
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh.
Dkt.Hamisi Kigwangalla akifurahia jambo pamoja na Waziri wa Uwekezaji
wa Oman Mhe. Salem Ben Nasser Al Ismaily, alipokuwa akiwasili kwenye
tukio la Ngoma na nyimbo za Taifa la Oman, Jijini Dar es salaam jana
Oktoba 18, 2017
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh.
Dkt.Hamisi Kigwangalla akiteta jambo pamoja na Waziri wa Uwekezaji wa
Oman Mhe. Salem Ben Nasser Al Ismaily, wakati akishuhudia tukio la Ngoma
na nyimbo za Taifa la Oman, Jijini Dar es salaam jana Oktoba 18, 2017
Bendi ya Jeshi la Taifa la Oman wakipiga nyimbo za Taifa hilo zinazofanyika wakati wa vita na ukombozi
Baadhi ya wananchi wakiwa na bendera za Taifa la Oman na Tanzania wakishuhudia tukio hilo
Baadhi ya Askari Maji wa kikosi cha Oman wakiwa katika tukio hilo.
Dkt. Kigwangalla akizungumza na wanahabari (Hawapo pichani)
Wachezaji wa Oman wakionesha ngoma za Utamaduni wa Taifa hilo.
…………….
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh.
Dkt.Hamisi Kigwangalla amesema Tanzania na Nchi ya Oman zimefanya
mazungumzo katika kuimalisha sekta ya Utalii hasa kwenye Utalii wa
kukuza Utamaduni na ule wa Kihistoria uliokuwepo miaka mingi kwa Mataifa
hayo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.
Kigwangalla amebainisha hayo jioni ya jana Oktoba 18,2017, wakati
alipokuwa mgeni rasmi kwenye maonyesho ya nyimbo na ngoma za Taifa la
Oman yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam
ambapo pia tukio lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri
na viongozi wa Taifa hilo la Oman ambao wapo Nchini kwa ziara ya
kusambaza Ujumbe wa Amani na Upendo kupitia meli ya kifahari ya Mfalme
wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ‘Fulk Al Salamah’.
Akizungumza mara baada ya
kushuhudia maonyesho ya ngoma na nyimbo hizo za Taifa la Oman, Dkt.
Kigwangalla amebainisha kuwa, Watanzania wameweza kujifunza na kufurahia
utamaduni wa Oman hasa kupitia nyimbo, ngoma na mashahiri ambapo
amebainisha kuwa Serikali itaendeleza ushirikiano mwema hususani wa
Kiutaduni na kukuza Utamaduni.
“Watanzania na watu wa Taifa la
Oman ni ndugu. Hivyo kupitia ngoma na nyimbo hizi walizoonesha hapa
zinafanana sana za zile za Visiwa vya Zanzibar na ukanda wetu huu wa
Pwani wa Tanzania.
Pia hata baadhi ya viongozi
waliokuja na msafara huu wanazungumza vizuri lugha ya Kiswahili bila
kuchanganya na lugha nyingine huku wengine kama mulivyowaona wana asili
ya Tanzania ikiwemo Visiwa hivyo vya Zanzibar ambapo walizaliwa huko.”
Ameeleza Dkt. Kigwangalla.
Aidha, ameeleza kuwa, kwa sasa
wanakusudia kutengeneza chanzo kipya cha Utalii ambacho kitakuwa ni cha
Kihistoria na Kiutamaduni baina ya Mataifa hayo mawili na kufafanua
kuwa, Histoia ya Tanzania hasa Lugha ya Kiswahili huwezi kukitenganisha
Bara la Arab hususani watu wa Oman.
“Kuna wengine wasomi wa Historia
na utamaduni wa Uislamu wamebainisha kwenye taarifa za kisayansi, kuwa
pengine hata dini ya kiisilamu ilianza kufika ukanda wa Pwani wa Afrika
Mashariki kabla ya hata haijafika baadhi ya Nchi ya Mashariki ya Kati.
Hii ni pamoja na makaburi ya kale
kule Bagamoyo, Pemba na sehemu nyingine za Tanzania ambapo kwa pamoja
yanaonesha uwepo wa Waislamu na mashekhe wa kiisilamu waliofika kuanzia
mwaka 1200 mpaka hadi 2000, miaka mingi iliyopita.” Alibainisha Dkt.
Kigwangalla.
Ameongeza kuwa: “Wao wakitangaza
vivutio vyao, watavitangaza na vivutio vyetu vya Tanzania. Lakini pia
sisi tutatumia fursa vivutio tulivyonavyo ambavyo wao hawana kama Mbuga
za Wanyama kuwaalika watu wa Omani kuja kutalii Tanzania, kipindi cha
Mwezi Juni, Julai hata Agosti wao ni kipindi cha joto kali kwani wakati
mwingine msimu huo kule wao wanakuwa na utaratibu wa kutoa rikizo ama
mapumziko ya muda wa zaidi ya siku 30 hadi 40 hivyo tutatumia fursa ya
kipindi hicho na hata wale wanaowapokea Oman waweze kuja Tanzania
kutalii” alieleza.
Pia alimalizia kwamba, ushirikiano huo, utaongeza soko kubwa la kiutalii.
Msafara huo wa viongozi wa Oman
wakiwemo Mawaziri na wafanyakazi wa Meli hiyo ya Mfalme wa Taifa hilo
unajumuisha watu zaidi ya 300 ambapo leo Oktoba 19,2017, umetembelea
Wilaya ya Bagamoyo kujinea fursa za kiuwekezaji na uchumi katika ukanda
huo wa Pwani huku Meli hiyo kesho Oktoba 20,2017 ikitarajiwa kuondoka
kuelekea Mombasa Nchini Kenya.
EmoticonEmoticon