Mkurugenzi wa Huduma za
Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCD), Dkt. Abdulsalaam Omar, akimfafanulia mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo lililoko kwenye hema kubwa la Jakaya Kikwete, kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam 2017, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kuhusu hatua ambazo mfanyakazi anapaswa kuchukua baada ya kupata maradhi au kuumia wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi kabla ya kupatiwa Fidia na WCF.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akizungumza wakati akiwa kwenye banda la Mfuko huo |
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAAJIRI na wafanyakazi wamejitokeza
kwa wingi kupata elimu kuhusu kazi za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF),
kwenye banda la Mfuko huo lililoko kwenye hema kubwa la Jakaya Kikwete kwenye
viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam
kunakofanyika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam.
Maonesho hayo ya kila mwaka huwaleta
pamoja wafanyabiashara ya makampuni makubwa ya kimataifa kutoka nje na dnani ya
nchi, lakini pia kunakuwepo na mkusanyiko mkubwa wa wafanyakazi wa umma na
binafsi wanaotoa huduma mbalimbali kwa watu wanofika kutembeela maonesho hayo.
Mfuko wa Fidia kwa wWafanyakazi,
(WCF) imetumia fursa hiyo kutoa elimu kwa waajiri na wafanyakazi ambao walifika
kwenye banda la Mfuko huo na kupatiwa maelezo ya kina kuhusu kazi za Mfuko
kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wake Bw. Masha Mshomba, wakurugenzi na wakuu wa
idara pia.
“WCF ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
ulioanzishwa kwa mujibu wa sheria namba 5 ya Fidia kwa Wafanyakazi kifungu
namba 263 ya mwaka 2015.” Bw. Mshomba aliyasema hayo akiwa kwenye banda hilo
ambapo waajiri na wafanyakazi walifika kupata elimu zaidi ya kuhusu Mfuko huo.
Bw. Mshomba aliendelea kufafanua
kuwa, kwa mujibu wa sheria iliyoanzasha Mfuko huo, tofauti na Mifuko mingine ya Hifadhio ya Jamii, ambapo mwajiri na mfanyakazi hutoa michango ya kila mwezi, kwa upande wa WCF, ni mwajiri pekee ndiye anawajipika kumchangia mfanyakazi wake kila mwezi na mfanyakazi hawajibiki kutoa mchango wowote. Aidha Bw. Mshomba alieleza kuwa, dhumuni kuu la kuanzishwa kwa Mfuko huo ni kutoa Mafao ya kutosha na stahili kwa Mfanyakazi aliyepatwa na maradhi au
majeraha yaliyotokana na kazi anazozifanya Mfanyakazi huyo.
“Na ifahamike kwamba, Mafao haya
analipwa Mfanyaakzi aliyepatwa na madhara hayo imma wakati akiwa kazini au
madhara hayo yanapojitokeza hata baada ya kuacha kazi ilimradi madaktari
wathibitishe kuwa madhara hayo yametokana na kazi alizokuwa akifanya au kifo
ambapo watalipwa wategemezi wake.” Alifafanua Bw. Mshomba.
Miongoni mwa Mafao ambayo Mfuko
utatoa kwa Mfanyakazi aliyepatwa na maradhi au majeraha ni pamoja na fao la
matibabu, Fidia kwa ulemavu wa muda, (Temporary disability), Msaada wa
uangalizi wa kudumu, Msaada wa mazishi kwa mfanyakazi aliyefariki kutokana na
kazi aifanyayo, lakini pia Fidia kwa wategemezi wa marehemu aliyepatwa na
umauti akiwa kazini.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za
Tiba na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulsalaam Omar, alisema
Mfanyakazi aliyeumia kutokana na kazi aifanyayo au maradhi yaliyosababishwa na
kazi aifanyayo, Mfuko utagharimia huduma za gari la kubeba wagonjwa, kumuona
daktari, upasuaji, pamoja na matibabu kwa ujumla baada ya kufanyiwa tathmini na
madaktari ambao tayari wamepatiwa mafunzo ya namna ya kufanya tathmini kwa
Mfanyakazi aliyeumia au kupata maradhi kutokana na kazi anayoifanya.
Naye Mkuu wa kitengo cha Mawasilianonna
Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge, aliwahimiza waajiri na wafanyakazi
kutembelea banda hilo ili kupata elimu lakini pia kujua haki za Mfanyakazi na
mwajiri pia.
“Mfulo huu unatoa nafuu sio tu
unasaidia Mfanyakazi kulipwa Fidia Stahili bali pia unatoa nafuu kwa mwajiri
kwani ghara hizo zitasimamiwa na WCF na sio Mwajiri. “Ndio maana tunawahizimiza
waajiri kote nchini kutoka sekta binafsi na umma, kutoa michango ya kila mwezi
kama sheria inavyotaka.” Alisema Bi. Laura.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na
Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge, (kulia), akizungumza na Posta Masta Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Deo Kwiyukwa, wakati alipotembelea banda hilo.
Mkurugenzi wa Huduma za
Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCD), Dkt. Abdulsalaam Omar,
akimfafanulia mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo lililoko
kwenye hema kubwa la Jakaya Kikwete, kwenye maonesho ya 41 ya biashara
ya kimataifa ya Dar es Salaam 2017, barabara ya Kilwa jijini Dar es
Salaam kuhusu hatua ambazo mfanyakazi anapaswa kuchukua baada ya kupata
maradhi au kuumia wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi kabla ya
kupatiwa Fidia na WCF.
Wafanyakazi hawa wakipatiwa maelezo mbalimbali yahusuyo huduma zitolewazo na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), walipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam
Afisa Uhsuiano Mwandamizi wa WCF, Bw. Sebera Fulgence, (wapili kushoto), akimpatia maelezo mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, (kushoto), akizunguzma jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Elimu wa Mamlaka ya Udhibiti Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Bi. Saraha Kibonde Msika, ambaye alitembelea banda hilo. SSRA imeweka maafsia wake kila banda linalotoa huduma ya hifadhi ya jamii kwenye maonesho ya mwaka huu.
Afisa wa WCF, (kulia), akimuhudumia mwananchi huyu aliyefika kwenye banda la WCF
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na
Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge, (kushoto), akimsikilzia mwananchi huyu aliyefika kwenye banda la Mfuko huo.
Afisa wa WCF, Bi.Inocencia William, (kulia), akimpatia maelezo yenye kuhusu huduma za WCF mwananchi huyu aliyefika kujua nini hasa kazi ya Mfuko huo na faida zake kwa Mfanyakazi na Mwajiri
Bw. Mshomba, (kulia), akiongongozana na Bi Laura, (kushoto) wakati akiwasuli kwenye banda hilo ili kuwahudumia wananchi. Kushoto ni Sebera Fulgence, Afisa Uhusiano mwandamizi wa Mfuko.
EmoticonEmoticon