- Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa tawi jipya la Kampuni ya Plus Events Cards, Mwenge Sokoni wauzaji wa kadi mbalimbali na maua ya maharusi jumla na rejareja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Plus Events Cards, Bi. Rehema Moses na Mkurugenzi Mkuu, Raimond Njuu (kushoto) wakishuhudia.
- Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel (katikati) akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Plus Events Cards, Raimond Njuu (kushoto) mara baada ya kuzindua tawi jipya la Kampuni ya Plus Events Cards, Mwenge Sokoni wauzaji wa kadi mbalimbali na maua ya maharusi jumla na rejareja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Plus Events Cards, Bi. Rehema Moses akishuhudia.
- Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Plus Events Cards, Bi. Rehema Moses (kushoto) akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel (kulia) sehemu ya bidhaa zinazouzwa na duka hilo mara baada ya kuzinduliwa. Kampuni ya Plus Events Cards, wauzaji wa kadi mbalimbali na maua ya maharusi jumla na rejareja imezinduwa tawi jipya Mwenge Sokoni jijini Dar es Salaam.
- Hapa ikikatwa keki ya pongezi na viongozi wa Kampuni ya Plus Events Cards.
- Picha ya pamoja ya wageni waalikwa baada ya uzinduzi
Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI Mkuu
wa Taasisi ya Doris Mollel, Bi. Doris Mollel amezinduwa tawi jipya la
duka la kadi la Kampuni ya 'Plus Events Cards' Mwenge, Sokoni Jijini Dar
es Salaam huku akiwataka wajasiliamali wadogo na wakubwa wauzaji wa
bidhaa hizo kujitokeza kuchangamkia fursa hiyo ili wajipatie kipato. Bi.
Mollel ametoa kauli hiyo alipokuwa akizinduwa tawi hilo,
linalofunguliwa kusogeza huduma za uuzaji kadi za kisasa jumla na
rejareja kwa wananchi eneo hilo.
Pamoja
na hayo, Bi. Doris Mollel aliwashauri wananchi kupenda kununua bidhaa
halisi na kuachana na bidhaa feki kwani zimekuwa na madhara huku
zikilikoseshea taifa mapato. Alisema bidhaa nyingi feki haziingii kwa
utaratibu rasmi nchini hivyo licha ya madhara kwa watumiaji zimekuwa
zikilikosesha taifa mapato.
"...Nashauri
Watanzania wenzangu tupende kununua bidhaa halisi zinazoendana na
thamani ya fedha tunazotoa. Uzuri sasa hivi wauzaji wengine wamekuwa
wawazi wanakwambia hii ni bei rahisi kwa kuwa ni feki na hii ndio bidhaa
halisi...tujenge utamaduni wa kutumia bidhaa bora na halisi kwa manufaa
yetu na taifa," alisisitiza Bi. Doris Mollel.
Aidha
aliipongeza kampuni ya Plus Events Cards wauzaji wa kadi na maua ya
maharusi kwa kusogeza huduma zake eneo la Mwenge na kutoa fursa kwa
wajasiriamali kuwatembelea kwa ajili ya kusambaza bidhaa hizo Dar es
Salaam na hata mikoani. Aliongeza kuwa hatua hiyo si tu imesogeza huduma
kwa wahitaji bali imetoa fursa kwa wajasiriamali wadogo kupata bidhaa
za kadi kirahisi na kuzisambaza kwa wahitaji.
- Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Plus Events Cards, Bi. Rehema Moses (kushoto) akimlisha keki ya pongezi Mkurugenzi Mkuu, Raimond Njuu (kushoto) mara baada ya uzinduzi.
- Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Plus Events Cards, Raimond Njuu (kulia) akiwashukuru baadhi ya wageni waalikwa mara baada ya uzinduzi wa tawi lao lililopo Mwenge Sokoni wauzaji wa kadi mbalimbali na maua ya maharusi jumla na rejareja jijini Dar es Salaam.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Plus Events Cards, Bi.
Rehema Moses ameiomba Serikali kujenga mazingira ya ulipaji kodi na
malipo anuai ya vibali vya biashara kufanyika eneo moja ili kupunguza
urasimu ambao wamekuwa wakiupata wafanyabiashara wanapoitaji kulipia
tozo hizo. Mkurugenzi huyo Mtendaji alitoa kauli hiyo kwenye uzinduzi wa
tawi jipya la uuzaji kadi jumla na rejareja kwa ajili ya matukio
mbalimbali ya sherehe eneo la Mwenge, Sokoni jijini Dar es Salaam.
Bi.
Moses alisema wapo wafanyabiashara waadilifu ambao wanajua umuhimu wa
kulipia tozo mbalimbali na vibali vya biashara wanazozifanya lakini
baadhi wamekuwa wakikwazwa na urasimu uliopo katika ufuatiliaji wa
vibali hivyo na mtawanyiko wa ofisi anuai za kufanyia malipo, jambo
ambalo linachangia kujikuta wanashindwa kulipia kwa wakati.
Mfanyabiashara
huyo mwanamama na Mtanzania wa kwanza kusambaza bidhaa hizo za kisasa
aliiomba Serikali kuangalia uwezekano wa vibali vyote na malipo kuwa
yakifanyika eneo moja ili kumrahisishia mfanyabiashara kukamilisha
vibali husika kwa wakati, na kumpunguzia mfanyabiashara vikwazo ambavyo
wakati mwingine vimekuwa vikimpotezea muda mwingi katika ufuatiliaji.
Aidha
alivishauri vyombo vya kudhibiti ubora wa bidhaa kuongeza nguvu ili
kudhibiti baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakichapisha kadi
feki nchini na kuwalaghai watanzania kuwa ni halisi, jamboa ambalo
linawaharibia wafanyabiashara wanaosambaza bidhaa halisi. Alisema
kampuni yake ambayo imekuwa ikisambaza kadi za kisasa za matukio
mbalimbali ya sherehe jumla na rejareja kutoka nchini China ipo tayari
kuwasaidia wajasiliamali waaminifu kutoka popote nchini kufanya biashara
hiyo bila udanganyifu ili kumpatia mlaji wa mwisho bidhaa halisi kwa
bei nzuri.
- Kulia ni mfanyakazi wa Kampuni ya Plus Events Cards, akimuonesha mmoja wa wateja baadhi ya bidhaa mara baada ya uzinduzi huo.
- Picha ya pamoja ya wageni waalikwa baada ya uzinduzi
______________________________ ______________________________ _______________________
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com
http://joemushi.blogspot.com
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com
http://joemushi.blogspot.com
EmoticonEmoticon