Wakati
kesho Jumatano Julai 5, 2017 timu yetu ya Tanzania ya mpira wa miguu -
Taifa Stars ikicheza na Zambia katika Nusu Fainali ya kuwania Kombe la
Castle COSAFA, Kocha Mkuu Salum Shaban Mayanga amemuongeza kwenye kikosi
Mshambuliaji John Raphael Bocco.
Bocco
kwa sasa yuko Afrika Kusini pamoja na timu hiyo akichukua nafasi ya
Mshambuliaji Mbaraka Yussuf Abeid aliyejepata majeruhi kwenye michuano
hiyo iliyoanza Juni 25, mwaka huu ambako Tanzania ilikuwa Kundi ‘A’
pamoja na timu za Malawi, Mauritius na Angola.
Tanzania
iliibuka kinara katika kundi hilo na kucheza Robo Fainali ambako
ilicheza na Afrika Kusini na kuitoa katika hatua hiyo hivyo kwa mujibu
wa ratiba, kesho Jumatano Julai 5, mwaka itashindana na Zambia.
Kocha
Salum Mayanga amefafanua kuwa mbali ya Bocco kujaza nafasi hiyo,
amemwongeza kwenye kikosi ili kuongeza nguvu ya kupambana na Rwanda
katika mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa
wachezaji wanaocheza ligi za ndani - CHAN.
Mchezo
dhidi ya Rwanda utafanyika Julai 15, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza. Mchezo wa marudiano utafanyika baadaye mwezi huu
au mapema mwezi ujao na mshindi wa jumla atacheza na Uganda. Mshindi wa
jumla kati ya Tanzania na Uganda ndiye atakayefuzu kwa fainali za CHAN
zitakazofanyika Kenya, mwaka 2018.
EmoticonEmoticon