Jijini Dar es salaam leo Jumanne tarehe 4 Julai 2017, Kampuni inayoongoza ya maisha ya kidigitali, Tigo Tanzania, baada ya mafaniko ya promosheni ya Jaza Ujazwe, sasa inaendelea na promosheni za kusisimua zaidi ya Jaza Ujazwa, Ujaziwe Zaidi ambapo wateja watakuwa wanaendelea kupokea bonas za papo kwa hapo kwa kushiriki katika droo za kila siku na kila wiki ambazo zitatoa zawadi za bure za muda wa maongezi, data na Ujumbe mfupi kwa washindi kwa muda wa mwaka mzima pamoja na smartphone za Samsung S8. Wanachotakiwa kufanya wateja wote ni kuongeza salio kwa njia ya vocha za kukwangua, Tigo Pesa au Tigo Rusha.
Promosheni hii imekuwa gumzo hapa jijini baada ya kampuni ya mawasiliano ya simu ya Tigo kuamua kuigia katika mitaa ya jiji la Dar es salaam na kutoa simu ya smartphone ya kisasa ya Samsung S8 ambayo ina GB 30, dakika 3,000 na SMS 3,000 kila mwezi kwa mwaka mzima. Kwa mujibu wa Tigo, promosheni hii imekuja sokoni kama sehemu ya kampeni ya ‘Jaza Ujazwe’ ambayo ni shukurani kwa wateja wa Tigo kwa uaminifu wao usiobadilika kwa kampuni hiyo.
Mpaka sasa, wateja wenye bahati wapatao 36 kutoka sehemu mbalimbali nchini wameibuka washindi katika droo za kila siku na kila wiki, ambapo baadhi yao wameondoka na muda wa maongezi usio na kikomo na data za kutumia mwaka mzima.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni za Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi kwenye mitaa katika viwanja vya Tegeta Nyuki, Kaimu Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo, Bwana William Mpinga amesema “Tigo inathamini mchango mkubwa ambao wateja wetu wamekuwa wanatupatia kwa muda wa miaka mingi, hii ndio sababu tunaamini kwamba wanapaswa kupewa shukurani kwa uaminifu wao endelevu. Kama kampuni tuna furaha kuwa zawadia wateja wetu kwa mara nyingine ili kuwawezesha kuendelea kufurahia huduma zetu zenye ubora wa hali ya juu.”
Zaidi ya kupata washindi wa kila siku na kila wiki, tumeamua kupeleka promosheni yetu mitaani na kuongeza fursa ya wateja wetu kushiriki katika uzinduzi wetu unaoambatana na burudani kutoka kwa msanii maarufu Joti na kushinda Samsung S8 ambayo inakuja na GB 30, dakika 3,000 na SMS 3,000 kila mwezi kwa muda wa mwaka mzima.
Mpaka sasa Lukinga Hamisi kutoka Kigamboni, Musa Banji kutoka Karume na Rajabu Mabela wa Mbagala wamejishindia kila mmoja simu ya Samsung S8 kutoka katika uzinduzi wa unaoendelea mitaani na pia watapokea GB30, dakika 3,000 za muda wa maongezi na SMS 3,000 kila mwezi kwa muda wa mwaka mzima.
Mpinga alibainisha kwamba promosheni mpya ita imarisha Tigo kuwa ndio kampuni inayotoa bidhaa na huduma zenye bei nafuu, wakati huo huo itakuwa inaimarisha jukumu lake kama kampuni ya mawasiliano yenye ubunifu zaidi Tanzania.
“Promosheni hii imekuja kufuatia uboreshaji wa miundombinu ya mtandao wetu uliofanyika hivi karibuni ambao unahakikisha utendaji wa hali ya juu wa utoaji wa huduma. Kwetu sisi Tigo, kila wakati tunakuwa wabunifu katika kutengeneza mbinu mpya za kusisimua ambazo zinazoimarisha uhusiano wetu na wataja wetu. Promosheni hii ya uaminifu ni njia bora ya kuwazawadia na kuwashukuru wateja wetu kwa kuendela kutumia huduma na bidhaa zetu.” Alisema Mpinga.
Alithibitisha tena kwamba Tigo imekusudia kuendelea kuwazawadia wateja wake kwa bidhaa na huduma za kusisimua zaidi na akaongeza kwamba “ Ubunifu wa huduma na bidhaa zetu unatokana na utafiti wa kina unaolenga kuwaridhisha wateja wetu. Kwa hiyo Jaza Ujazwe, Ujaziwe zaidi inakuja kukabiliana na mahitaji ya wateja ya kuwa na hisia ya msisimko kila mara wanapo tumia huduma zetu. Tunaamini kwamba wateja wetu watafurahia dakika, SMS au data za ziada wanazo zawadiwa kila mara wanapoongeza salio na hivyo itaboresha mwenendo wa mawasiliano yao” alielezea Mpinga
EmoticonEmoticon