Kamati
ya Utendaji (EXCOMM) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania,
imekutana tena leo Jumanne Julai 4, 2017 katika kikao cha dharura ambako
ilijadili mgawanyiko katika Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
Kamati
hiyo ya utendaji inakutana kwa dharura kwa mujibu wa Ibara ya 35 (1) ya
Katiba ya TFF inayosomwa pamoja na Ibara ya 35 (6). Kikao cha Kamati
hiyo kilianza saa 8.58 alasiri hadi saa 10.51 jioni.
Katika
kikao chake kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za shirikisho, Karume
jijini Dar es Salaam Kamati iliamua kufanya mabadiliko madogo katika
Kamati zake za Kisheria na Kamati za uchaguzi kwa mujibu wa Katiba Ibara
ya 44 (7) na Ibara ya 52 inayotoa mamlaka ya kufanya mabaduiliko hayo.
Katika
Kamati ya Uchaguzi, EXCOMM imeteua Mawakili kuongoza kamati hiyo
wakiongozwa na Msomi Wakili Revocatus Kuuli; Mheshimiwa Wakili Mohammed
Mchengelwa; Msomi Wakili Malangwe Mchungahela; Msomi Wakili Kiomoni
Kibamba na Msomi Wakili Thadeus Karua.
Katika
Kamati ya Rufaa Uchaguzi, EXCOMM imeteua Msomi Wakili, Abdi Kagomba
kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Msomi Wakili Kenneth Mwenda
na wajumbe ni Msomi Wakili Rashid Sadalla, Mhe. Jabir Shekimweri na
Mohammed Gombati.
Kadhalika
katika kamati za kisheria za TFF, ikianzia Kamati ya Maadili, EXCOMM
imeteua Msomi Wakili Hamidu Mbwezeleni kuwa Mwenyekiti wakati Makamu
Mwenyekiti ni Msomi Wakili Steven Zangira na wajumbe ni Mhe. Glorius
Luoga, Walter Lungu na Amin Bakhressa.
Kamati
ya Rufaa na Maadili, EXCOMM imeteua Msomi Wakili Ebenezer Mshana kuwa
Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Naibu Kamisha katika Jeshi la
Polisi (DCP), Mohammed Mpinga na Wajumbe ni Msomi Wakili Benjamin
Karume; Dk. Lisobine Kisongo na Mrakibu Msaidizi wa Polisi - ASP
Benedict Nyagabona.
Kamati
ya Nidhamu ya TFF, EXCOMM imeteua Tarimba Abbas kuwa Mwenyekiti wakati
Makamu Mwenyekiti ni Peter Hella huku Wajumbe wakiwa ni Boniface
Lyamwike, Dk. Billy Haonga na Kassim Dau.
Kamati
ya Rufaa ya Nidhamu, EXCOMM imeteua Msomi Wakili Rahim Shaban kuwa
Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Siza Chenja huku Wajumbe wakiwa
ni Abbas Mtemvu; Amani Mulika, Amin Bakhressa na Stella Mwakingwe.
EmoticonEmoticon