Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiandaa mti kwa ajili
ya kuupanda ikiwa ni jitihada za kuunga mkono kampeni ya upandaji miti
nchini. Zoezi hilo limefanyika leo katika Halmashauri ya mji Korogwe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na wawakilishi
wa wananchi, watumishi na Watendaji wa Halmashauri ya Mji Korogwe
(hawapo pichani). Waziri Makamba amesisitiza umuhimu wa kutunza vyanzo
vya maji na hifadhi ya mazingira kwa ujumla wake.
Sehemu ya wawakilishi wa
wananchi, watumishi na Watendaji wa Halmashauri ya Mji Korogwe
wakimsikiliza Waziri Makamba alipofanya ziara ya kikazi kutembelea
Halmashauri hiyo, kusikiliza na kujionea changamoto za kimazingira na
kuainisha namna bora ya kukabiliana nazo.
…………………………………………………………………………………..
Akizungumza katika katika ziara
yake mkoani Tanga iliyoingia siku ya tano Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Mhe. January Makamba amesema kuwa ni vema rasilimali za
nchi hii zitunzwe kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.”hatuwezi
kufanikiwa kama tutaharibu mazingira” Makamba alisisitiza.
Waziri Makamba amesema ofisi yake
ya imedhamiria kuchukua swala la mazingira kwa uzito wa kipee ikiwa ni
pamoja na kuweka hifadhi ya mazingira katika mipango ya maendeleo.”
Uwekezaji wote lazima uende sambamba na hifadhi ya mazingira”
Aidha, uongozi wa Halmashauri ya
Mji Korogwe imetakiwa kuwachukua hatua kali wananchi wote wanaofanya
shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji, kwa kutumia sheria ya
Mazingira ya mwaka 2004 na ile ya maji ya mwaka 2009. Waziri Makamba
amesema kuwa ofisi yake iko katika hatua za mwisho za kuteua wakaguzi wa
mazingira 200 ambao watapata mafunzo na kusambazwa katika Halmashauri
mbali mbali nchini.
Pia Waziri Makamba amesema kuwa
katika kikao kijacho cha Bunge Ofisi ya Makamu wa Rais itatoa waraka juu
ya usimamizi na uchimbaji wa mchanga nchini pamoja na umiliki wa
“Chain-saw” kwa lengo kuweka utaratibu utakaowezesha kutambua na kutoa
vibali maalumu kwa shughuli hizo ili kulinda mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Mhe. January Makamba ameendelea na ziara yake maalumu ya kukagua
shughuli mbalimbali za kimazingira nchini na hii leo amepokea taarifa
ya hali ya mazingira katika Halmashauri ya Mji Korogwe na Same.
Awali akimkaribisha Waziri
Makamba, Mwenyekiti wa Halmashauri ya hiyo Bw. Hillary Ngonyani amesema
kuwa katika kutekeleza sheria ya mazingira zoezi la uzoaji na utupaji wa
taka ngumu na taka maji umewekewa mkakati maalumu na kutekelezwa
kikamilifu pia usafi wa mazingira umefanyika kwa kufanya ukaguzi wa
nyumba hadi nyumba na kutoza faini kwa wananchi wasio na vyoo.
Bw. Ngonyani amebainisha kuwa
wananchi wanaokiuka taratibu hizo hushtakiwa kwenye mabaraza ya kata na
kupewa muda maalumu wa kujenga vyoo, kusisitizwa kuvitumia pia kuamriwa
kusafisha mazingira yao chini ya uangalizi wa maafisa afya.
Aidha Bw. Ngonyani amesema kuwa
wananchi wamekumbusha pia kutofanya shughuli za maendeleo kando ya mito
na vyanzo vya maji ili kupunguza athari kwa mazingira, na kuunda kwa
kamati za mazingira.
Katika hatua nyingine Bw.
Ngonyani ameinisha changamoto zinazojitokeza katika Halmashauri ya
Korogwe mji kuwa ni pamoja na Ukosefu wa wakaguzi wa Mazingira na athari
za mabadiliko ya tabianchi yanayosababisha vipindi vya mvua kubadilika
na kuongezeka kwa joto.
EmoticonEmoticon