Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ziara ya kushtukiza
katika Bandari ya Dar es Salaam kufatilia maagizo yake ya kudhibiti
vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na wafanyabiashara wanaogiza na
kusafirisha mizigo ndani na nje ya nchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihesabu makontena 20 yenye
mchanga wa madini ambapo ameamuru kontena hizo zisisafirishwe mahali
popote.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na kutoa maagizo
mbalimbali kuhusu makontena 20 (yanayoonekana nyuma) yenye mchanga wa
madiniuliokuwa usafirishwe kwenda nje ya nchi ambapo ameagiza Kontena
hizo zisisafirishwe mahali popote.
Makontena 20 yenye mchanga wa
madini yakiwa yamezuiwa kusafirishwa nje ya nchi na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara alipofanya ziara
ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam.
Picha namba 12. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikagua nyaraka
mbalimbali zenye maelezo kuhusu makontena ambayo husafirishwa nje ya
nchi katika Bandari ya Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia baadhi ya magari
yalivyoingizwa nchini na Wafanyabiashara wakubwa kwa njia isiyo halali
ya kudai kuwa ni makontena ya mitumba wakati ndani yake wanaficha magari
yakifahari wanayoyachanganya na bidhaa zilizochakaa.
Moja ya kontena likiwa lina gari
ndani yake aina ya Range Rover ambapo muagizaji alidai kuwa anaagiza
mitumba lakini kumbe ndani yake anakuwa ameficha magari ya kifahari.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na IGP Ernest
Mangu mara baada ya kufanya ukaguzi Bandarini hapo. PICHA NA IKULU
EmoticonEmoticon