Faida ya Hifadhi endelevu ya
Mazingira. Pichani ni kibanda maalumu kwa ajili ufugaji wa vipepeo
katika Kijiji cha Fanusi Wilayani Muheza. Wananchi wa eneo hilo wamekua
wakinufaika na uuzwaji wa vipepeo hao nje ya chini na kuboresha hali zao
za maisha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akipanda mti aina ya
‘Mnyasa’ katika kuunga mkono kampeni endelevu ya upandaji miti nchini,
katika Msitu wa Amani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akimsikiliza Bw. Richard
Kuyangana akiwasilisha maoni ya wananchi wa Hale katika Mkutano wa
Hadhara. Waziri Makamba amewataka wananchi hao kutii sheria, kanuni na
taratibu za hifadhi ya mazingira.
………………
Ziara maalumu ya Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. January Makamba kutembelea mikoa ya
Kaskazini mwa Tanzania yenye lengo la kung’amua changamoto za
kimazingira, athari za mabadiliko ya tabia nchi ili kuweka mikakati
sahihi ya kukabiliana na changamoto hizo, imeingi siku ya nne.
Hii leo Waziri Makamba ametembelea
Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, na kupokea taarifa ya hali ya Mazingira
Wilayani hapo taarifa iliyowasilishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhandisi
MwanaAsha Tumbo.
Bi Tumbo ameainisha changamoto za
kimazingira katika Wilaya yake kuwa ni pamoja na kuwa ni pamoja na Uvuvi
haramu, Mabadiliko ya tabianchi ambayo kwa kiasi kikubwa yanachangiwa
na shughuli za binadamu zisizozingatia uhifadhi endelevu ya mazingira
ikiwa ni pamoja na ukataji ovyo wa miti ya asili na misitu ya kupanda,
kilimo cha kuhamahama na uchimbaji wa madini katika kingo na pembezoni
mwa vyanzo vya maji.
Bi. Tumbo amesema kuwa hivi sasa
wilaya ya Muheza inakabiliwa na upungufu mkubwa wa mvua kutoka misimu
mitatu kwa mwaka hadi kufikia msimu mmoja tu. “katika siku za hivi
karibuni kumekua na ongezeko kubwa la uchimbaji holela wa madini
unaopelekea uharibifu mkubwa wa mazingira”. Ili kuimarisha doria
kikamilifu wakazi wa Wilaya ya Muheza wamewasilisha ombi maalumu la
kujengewa nyumba za askari hii ni baada ya kupata msaada kutoka United Nations Development Programme ambao wamekubali kujenga kituo cha polisi.
Aidha, jitihada mbalimbali
zimechukuliwa na uongozi wa Wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kuweka zuio
la ukataji miti hovyo. Miti iliyopigwa marufuku ni pamoja na miti
iliyooteshwa kwa juhudi za watu binafsi na hata ile ya
mashirika/taasisi. Kwa upande wake Waziri Makamba ameupongeza uongozi
wa wilaya hiyo kwa juhudi za dhati za kuhifadhi mazingira, pia
kuanzishwa kwa kampeni maalumu ya kupanda miti. Jitihada nyingine ni
pamoja na kufukia mashimo yote yaliyochimbwa na wachimbaji wadogo wadogo
wa dhahabu katika Kijiji cha Kihara, katika msitu wa Amani.
Katika siku hii ya nne Waziri
Makamba alipata fursa ya kutembelea “Amani Nature Researve” ambapo
alishuhudia ni kwajinsi gani mazingira yamehifadhiwa na kuchangia kwa
kiasi kikubwa mradi wa kuzalisha vipepeo na kuuza nje ya nchi biashara
ambayo imekua ikiwasaidia wakazi wa kijiji hicho katika kusomesha watoto
wao na kujenga nyumba bora za kuishi.
Wakazi hao wa kijiji cha Kata ya
Fanusi walianisha changamoto kubwa inayowakabili kwa sasa kuwa ni kukosa
soko la kuuza vipepeo hao baada ya kuzuiwa na Serikali.
“Niwahikikishieni kuwa suala hili tutalichukua na kulifikisha katika
Wizara husika na naamini litafanyiwa kazi mapema iwezekanavyo” Makamba
alisisitiza.
Nae Mhifadhi wa msitu wa Amani
Bi.Mwanaidi Kijazi ameainisha umuhimu huo kuwa ni pamoja na hifadhi ya
bionuai na mifumo ya ikojia, hifadhi ya viumbe hai adimu duniani,
maumbile ya asili maalumu kwa utunzaji wa vinasaba na chanzo kikubwa cha
vyanzo vya maji.
Ziara ya Waziri Makamba katika
mkoa wa Tanga hii leo imefanyika katika Wilaya ya Muheza ambapo
ameshiriki katika zoezi la kupanda miti, kutembelea misitu wa Amani na
kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kihara na kuwasisitiza
wakazi wa eneo hilo kutunza rasilimali zilizopo kwa manufaa ya sasa na
vizazi vijavyo.
Aidha, katika kuchangia shughuli
za maendeleo kijijini hapo Waziri Makamba ameahidi kununua miche ya miti
150,000 kwa ajili ya kuigawa maeno mbalimbali ya wilaya hiyo ikiwa ni
sehemu ya jitihada kwa wakazi hao kupanda miti kwa wingi kwa lengo la
kulinda na kutunza mazingira.
EmoticonEmoticon