Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na
Mazingira Mhe. Stanslaus Nyongo (Mb.) Maswa Mashariki akiongea na waandishi
wa Habari baada ya ukaguzi wa ujenzi wa ukuta wa Ocear Road katika Barabara
ya Baraka Obama Jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais
Bw. Richard Muyungi akiwasilisha taarifa utekelezaji wa ujenzi wa ukuta
wa fukwe ya Ocean Road kwa wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi malisili
na Mazingira. (Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)Sehemu ya ukuta wa fukwe ya Ocean Road kama unavyooneka katika picha ukiwa katika matengenezo. |
Evelyn
Mkokoi – Dar es Salaam
Kamati ya kudumu ya
Bunge ya Ardhi Maliasili na Mazingira, imetembelea mradi wa ujenzi wa ukuta
wa fukwe ya Ocean Road katika Barabara ya Barak Obama Jijini Dar es
Salaam, kwa lengo la kukagua mradi wa Mabadiliko ya Tabia nchi,
unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Akiongea na waandishi
wa Habari katika eneo la ujenzi wa ukuta huo, kaimu mwenyekiti wa
kamati hiyo Mhe. Stanslaus Nyongo (MB) Maswa Mashariki alisema kuwa
kuwa, kamati inaishauri serikali kutumia vizuri mahusiano ya nchi
yetu na wahisani ili kuweza kupata pesa za kusaidia suala zima la kuhimili
na kukabiliana na mbadiliko ya tabianchi.
Aidha, Mhe. Nyogo aliongeza
kwa kusema kuwa Serikali nayo iongeze jitihada za kupambana na
kukabiliana na athari na hasara zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi
kwa kutoa elimu ya kulinda mazingira kwa umma.
Kwa upande wake mjumbe
wa kamati hiyo Mhe Dk. Rafael Chegeni, alisema kuwa uharibifu wa mazingira
utokanao na ukataji miti ovyo kwa matumizi ya nishati ya mkaa ni mkubwa
na ndiyo unaopelekea athari kubwa za mabadiliko ya tabia nchi, na nishati
mbadala bado zinapatikana kwa gaharama za juu, na kushauri kuwa kuwe
na mikakati kwa serikali na sekta husika ya kumsaidia mwanachi wa kawada
kutunza mazingira aidha, kuwe na mkakati unaonekana na kusadia kuwa
na upatikani wa haraka wa nishati mbadala.
Baada ya wajumbe wa
kamati hiyo kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa upande wa
Dar es Salaam na Pwani, Mhe Hawa Mwaifunga alitaka kufahamu kuhusu
mradi wa majiko banifu, utekelezaji wake na ugawaji wa majiko hayo kwani
athari za mabadiliko ya tabia nchi yapo nchi nchi nzima.
Awali akiwasilisha ripoti
ya utelelezaji wa mradi wa mabadiliko ya tabia nchi unaohusisha ujenzi
wa ukuta wa ocean road, urejeshaji wa upandaji wa mikoko katika maeneo
ya mbweni, daraja la salenda, ununio na ujenzi wa mitaro katika maeneo
ya ilala Bungoni kata ya Buguruni, maeneo ya Mtoni katika Wilaya ya
Temeke na katika maeneo ya chuo cha Mwalimu Nyerere KIgamboni, Mkurugenzi
wa Idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi
, alisema kuwa takribani kiasi cha dola milioni 500 zinahitajika kila
mwaka nchini kwa ajili ya utekelezaji wa kazi hiyo ikiwa ni pamoja na
kusaidia mafunzo kwa wananchi katika ngazi za familia ili kuweza kukabilianda
na janga hili la mabadiliko ya tabia nchi.
Aliongeza kwa kusema kuwa
ujenzi huo wa ukuta wa ocean road utahusisha pia ujenzi wa njia za waendao
kwa miguu, viti vya kumpuzikia, na taa.
Mradi wa ujenzi wa ukuta
wa Ocean Rpoad unaoendelea kujengwa, umekalimika kwa asilimia 30% yenye
urefu wa mita 820, kwa pande nyingine kwenda juu kwa urefu wa mita 2.5,
na pande nyingine kwenda juu kwa urefu wa mita 4.
Mradi huo huo unafadhiliwa
na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) , na kusimamiwa na
shirika lingine la umoja wa maitaifa la Huduma kwa Miradi, (UNOPS) ambalo
linasimamia miradi yote ya mabadiliko ya tabia nchi duniani. Mradi huo
upo chini ya Uratibu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira. Na ujenzi
huo wa ukuta unafanywa na kampuni ya Dezo Civil Constractions ya jijjini
Dar es Salaam
EmoticonEmoticon