Katibu wa chama cha
mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama akiwa kwenye mmoja ya mikutano ya kampeni wa kumtafuta diwani wa kata ya Igombavanu wilayani mufindi akikitumikia chama.
Katibu wa chama cha
mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama akiwa kwenye mmoja ya mikutano ya kampeni akimwombea kura Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Maguli mwaka 2015 katika uwanjwa wa wambi mafinga.
Katibu wa chama cha
mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama akipeana mkono na waziri mkuu mstaafu wa awamu ya nne mh Mizengo Pinda kwenye moja ya majukumu ya kukitumikia chama.
Katibu wa chama cha
mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama akipeana mkono na Rais mstaafu wa awamu ya nne dr Jakaya Mrisho Kikwete na kubadilishana maneno ya hapa na pale
Na Fredy Mgunda, Mufindi
Na Fredy Mgunda, Mufindi
KATIBU wa chama cha
mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama ametangaza nia ya kugombea
nafsi ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa bunge la afrika mashariki kwa kuiwakirisha
Tanzania.
Akizungumza kwa njia ya simu Mhagama
alisema kuwa atahakisha lugha ya kiswahili inatumika barani afrika kama lugha
mama kwa kuwa ndio lugha ilisamba zaidi barani afrika.
“Nimetembea nchi nyingi hapa
afrika nimekutana na watu wengi wanazungumza Kiswahili hivyo hoja yangu itakuwa
kuahakikisha natimiza kitu alichotuachia hayati baba wa taifa mwalimu Julias
Kabarage Nyerere”.alisema Mhagama
Mhagama alisema kuwa
atalazimaka kuwatetea wakulima kwa kuwa asilimia kubwa ya watanzania wengi ni
wakulima na uchumi wetu bado unategemea kilimo hivyo ni lazima kuwekeza nguvu
kwenye kilimo chenye tija na kufanikiwa kuinua mazao yanayozalishwa hapa nchi
na kukuza uchumi.
“Tanzania tumebatika kuwa na
ardhi nzuri na kubwa ambayo kwa asilimia kubwa bado haijatumika kwa mjibu wa
wataalam wa kilimo hivyo ni lazima kutafuta nja mbadala ya kuwainua wakulima
hawa ili kuviwezesha viwanda vyetu kupata mali ghafi nyingi na za kutosha ili
kuinua kipato cha kila sekta hapa nchi”.alisema Mhagama
Aidha Mhagama amewataka
watanzania kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe
Magufuli kwa kazi anazozifanya kwa kutafuta njia bora ya kuinua uchumi wa
wananchi wake kutoka hapaulipo hadi kufikia uchumi wa viwanda kama sera yake
alivyoielekeza kwenye Tanzania ya viwanda.
“Angalia sasa tunapata
wawekezaji wengi kwenye sekta ya viwanda hii ni dalili nzuri ya kuukalibia
uchumi wa viwanda hivyo nikiwa mbunge wa bunge la Afrika Mashariki nitandelea
kuunga mkono Rais kwa kutafuta njia za kuwanua wawekezaji wazawa ili waboreshe
na kuanzisha viwanda vyao”.alisema Mhagama
Mhagama aliwaomba watanzania
kwa ujumla kumuombea ashinde kiti hicho ili aweze kuiwakirisha vyema nchi kwa
uadilifu uliotukuka
EmoticonEmoticon