Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini PEMBA Mhe Omar Khamis Othman
amesema ni jukumu la viongozi wa siasa kushirikiana na serikali kutatua kero
zinazowakabili wananchi katika maeneo yao .
Amesema kuwa viongozi wa majimbo wanashindwa kutambua wajibu
na majukumu yao hali ambayo inapelekea wananchi kukabiliwa na changamoto ambazo
zinaweza kutatulia na viongozi hao .
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mabandani Shehia ya
Ukunjwi Wilaya ya Wete waliofika Ofisini kwake kulalamikia ubovu wa barabara , amesema kuwa viongozi wa
majimbo wanao uwezo mkubwa kulipatia ufumbuzi .
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wananchi
wa Kijiji hicho kuendelea kuwa wastahamilivu wakati Serikali ya Mkoa
akifanya juhudi za kuwasiliana na watendaji kutoka Wizara ya Miundo
Mbinu na Mawasiliano ili waweze kuifanya matengenzo barabara hiyo na
kufanya iweze kupitika .
Kwa upande wao wananchi wa Kijiji hicho amesema kuwa
kutokana na ubovu wa barabara hiyo kunasababisha baadhi ya akinamama
wajawazito kujifungulia njiani wakati wakipelekwa kwenye Kituo cha Afya
na Hospitali .
Wamesema kuwa licha ya kero hiyo kuifikisha kwa Vingozi wao wa Jimbo , lakini badom ufumbuzi wake haujapatikana .
EmoticonEmoticon