Mkuu
wa mkoa wa Dar es slaam,Saidi Meck Sadiki(katikati) akiangalia athari ya
maji yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni jijini Dar
es slaam akiwa ameambatana na wakazi wa eneo hilo la Kunduchi
Ununio.Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na DAWASA inaendelea na
zoezi la kuyaondoa maji hayo pamoja na ujenzi wa mfereji mkubwa kuelekea
baharini utakaokusanya maji kutoka Bunju na Kunduchi na kuyapeleka
bahari ya Hindi.
Kazi ya ujenzi wa mfereji huo mkubwa wenye urefu wa kilometa 2.1 ikiendelea katika eneo la Kunduchi Ununio.
Maji
yaliyotuama yakiwa bado yamezingira nyumba na makazi ya watu eneo la
Boko jijini Dar es salaam ambayo harakati za kuyaoondoa zinaendelea
kufanywa na manispaa ya Kinondoni.
Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiki ( katikati ) akisikiliza
maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni Musa Nati wakati
akikagua utekelezaji wa zoezi la kuondoa maji katika makazi ya watu eneo
la Basihayo Tegeta.
………………………………………………………………….
Na.Aron Msigwa- MAELEZO
.Dar es Salaam.
Manispaa ya Kinondoni inaendelelea kujenga mfereji wa kudumu
wenye urefu wa Kilometa 2.1 ili kuondoa maji yaliyojaa kwenye makazi ya
watu, eneo la Basihayo -Tegeta,Bunju na Kunduchi na kuyapeleka bahari ya
Hindi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais alilolitoa hivi karibuni
mara baada ya kuwatembelea wananchi katika maeneo hayo walioathiriwa na
mafuriko.
Akitembelea maeneo yaliyoathiriwa na mvua hizo kujionea
utekelezaji wa agizo hilo leo, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki
Sadiki amesema kazi ya ujenzi wa mfereji huo utakaogharimu kiasi cha
shilingi milioni 900 inafanyika kwa kasi inayoridhisha licha ya ugumu
uliopo wa kutafuta uelekeo wa maji hayo kutoakana na uwepo wa makazi ya
watu.
Amesema ujenzi wa mfereji huo mkubwa unakwenda sambamba na
kazi ya uondoaji wa maji ya mvua yaliyojaa katika makazi ya watu katika
eneo la Basihaya inayofanywa na Shirika la maji Safi na Maji Taka Dar es
Salaam huku Manispaa ya Kinondoni chini ya usimamizi wa Muhandisi wake
Baraka Mkuya ikiendelea na uchimbaji wa mfereji wa juu na ule utakaopita
chini ardhi kuelekea baharini.
Amesema kuwa katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa
ufanisi mkubwa bila kuathiri makazi ya watu na kulazimika kulipa fidia
kwa wananchi Manispaa hiyo inaendelea kuzungumza na baadhi ya wananchi
ambao maeneo yao yatatumika kupitisha mfereji huo waruhusu kazi hiyo
iendelee huku taratibu nyingine zikiendelea kufanyika.
Aidha amesema kwa baadhi ya wananchi waliojenga kuta na
nyumba kwenye mkondo wa maji hususani eneo la Kunduchi Ununio na kuzuia
maji kuelekea baharini maeneo yao yatabomolewa na baadhi ya hati za
viwanja kufutwa.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mussa Nati akizungumza
mara baada ya kutembelea eneo hilo kushuhudia zoezi la uondoaji wa maji
na ujenzi wa mfereji huo amesema kuwa fedha zinazotumika katika kazi
hiyo zinatolewa na manispaa ya Kinondoni, na kazi hiyo itafanywa na
wataalam wa Manispaa hiyo na kufafanua kuwa kukamilika kwake kutaondoa
adha ya muda mrefu ya mafuriko waliyokuwa wanaipata wakazi hao kipindi
cha mvua.
“Manispaa ya Kinondoni tumetenga kiasi cha shilingi 900 kwa
ajili ya kufungua maji na kujenga mifereji ya kudumu inayoelekea
baharini katika ili wananchi waweze kuishi bila usumbufu wowote,na kazi
hii tutaimaliza ndani ya mwezi mmoja” Amesisitiza.
Naye Muhandisi wa Manispaa hiyo Baraka Mkuya amesema kuwa
kazi ya uondoaji wa maji na ujenzi wa mifereji ya wazi na ile inayopita
chini ya ardhi kutokea eneo la Basihayo Tegeta na kukatisha barabara ya
Bagamoyo kuelekea bahari ya Hindi urefu wa kilometa 2.1 itakamilika
ndani ya mwezi mmoja.
Kwa upande wao madiwani wa eneo hilo Bw.Majisafi
Sharifu,Diwani wa Kata ya Bunju (CHADEMA) na Bi.Janet Lite kupitia Chama
cha Mapinduzi (CCM) wamesema kazi ya utekelezaji wa agizo la Rais la
ujenzi wa mfereji huo inakwenda na kueleza kuwa itakuwa faraja kwa
wakazi wa kata hizo kutokana na adha kubwa ya mafuriko ya maji waliyokua
wanaipata wakati wa msimu wa mvua.
EmoticonEmoticon