MHE. KASSIM MAJALIWA AFUNGUA MAFUNZO YA HAKI ZA BINADAMU KWA WALIMU, WAKAGUZI NA WAKUFUNZI WA VYUO

May 19, 2015

1
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (OWM) – TAMISEMI (Elimu), Mhe. Kassim Majaliwa (MB) akifungua warsha ya mafunzo ya haki za binadamu kwa walimu wa shule za Sekondari, wakaguzi wa shule na wakufunzi wa vyuo vya ualimu katika hoteli ya Royal Village, mjini Dodoma leo. Mafunzo hayo yameandaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu chini ya Mradi wa utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu na kufadhiliwa na UNDP. Takriban washiriki 60 wanashiriki katika mafunzo hayo ya siku nne yanayotarajiwa kumalizika Mei 21, 2015. Washiriki hao wametoka mikoa ya Dodoma, Singida na Manyara, na hii ni warsha ya nne kufanyika.
2
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo ya mafunzo wakimsikiliza Mhe. Majaliwa.
3
Mwakilishi wa UNDP, Bw. Godfrey Mlisa akitoa salamu za ofisi yake wakati wa ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya haki za binadamu kwa waalimu wa shule za Secondari.
4
Mkurugenzi wa Elimu – Utawala kutoka TAMISEMI, Bw. Bernard Makali akitoa neno wakati wa ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya haki za binadamu kwa waalimu wa shule za Secondari.
5
Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Dk. Kelvin Mandopi akiongea muda mfupi kabla ya kumkaribisha Mhe. Naibu Waziri kutoa hotuba yake ya ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya haki za binadamu kwa waalimu wa shule za Secondari.
6
Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Dk. Kelvin Mandopi akimkabidhi Mhe. Majaliwa baadhi ya machapisho yaliyoandaliwa na Tume mara baada ya Mhe. Waziri kufungua rasmi Warsha ya mafunzo ya haki za binadamu kwa a waalimu.
7
Mhe. Kassim Majaliwa akibadilishana mawazo na Mwalimu Joachim Mpagama, mshiriki wa mafunzo hayo kutoka Wilayani Kongwa.
8
Mhe. Kassim Majaliwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na washiriki wa warsha ya mafunzo ya haki za binadamu kwa walimu wa shule za Sekondari, wakaguzi wa shule na wakufunzi wa vyuo vya ualimu.
(Picha zote na Germanus Joseph wa THBUB).

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »