Jamii yatakiwa kuwa na nidhamu katika shughuli za kujiletea maendeleo

May 19, 2015

so1
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Ester Riwa mbele akionyesha Sera ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 wakati wa mafunzo ya elimu ya Ujasiriamali, Mfuko wa Vijana, Stadi za Maisha na Uongozi bora kwa Vijana wa Halmashauri ya Tunduru.
so2
Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga aliyeshoosha mkono akiwa katika ukaguzi wa mradi wa kikundi cha Hatubanani kilichopo Halmashauri ya mji wa Tunduru kinachojishughulisha na duka la uuzaji wa vinywaji baridi, mradi wa kikundi hicho umepata mkopo wa shilingi milioni nne kutoka Idara ya Maendeleo ya Vijana.wa kwanza kushoto ni katibu wa kikundi hichi Bi Hawa Mayanga na kulia ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Vijana Sasanda kilichopo Mkoani Mbeya Bw. Laurian Masele.
so3
Maafisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiwa katika ukaguzi wa mradi wa ufugaji samaki kilichopo Halmashauri ya mji wa Tunduru wakati wa mafunzo kwa vijana ya kuwakwamua kiuchumi.Katikati ni Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Vijana Sasanda kilichopo Mkoani Mbeya Bw. Laurian Masele.
so4
Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga aliyeshoosha mkono akitoa mada ya jinsi ya utendaji kazi wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana wakati wa mafunzo ya kuwakwamua vijana wa Halmashauri ya Tunduru kiuchumi.
…………………………………………………………………………..
Jamii imetakiwa kuwa na nidhamu ikiwa ni pamoja na kuwa na usimamizi mzuri katika shughuli za kujiletea maendelo.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo kwa wajasiriamali vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bw. Manfred Hyera amesema chanzo cha mafanikio katika ujasiriamali nikuwa na nidhamu kwa jamii inayowazunguka kwani kwa kufanya hivyo kutawawezesha kuwaongezea kipato.
Bw.Hyera amesema kitendo cha baadhi ya wajasiriamali kutumia lugha chafu kwa wateja ndio chanzo kinachowarudisha nyuma na kufilisika kibiashara.
“Baadhi ya wajasirimali mnatumia lugha chafu kwa wateja wenu hiki ni chanzo kikubwa cha kufilisika kibiashara na kubaki kuilalamikia serikali”.Alisema.
Alisema serikali kupitia WizarayaHabari, Vijana, Utamaduni na Michezo inaniayadhati yakushirikiana na wanachi wote hususani Vijana ilikukabiliana na tatizo la ajira nchini.
Katika hatua nyingine AfisaVijana Bi. Amina Sanga amewashauri vijana kuwa wabunifu ili kuendana naushindani wa soko la biashara unaoendelea nchini na duniani kwa ujumla.
Akitolea mfano wa ujenzi unaoendelea wa barabara kwa kiwango cha lami Bi. Sanga alisema ni fursa mojawapo kwa vijana wa Halmashauri hiyo kubuni biashara ambayo itawaingizia kipato kiurahisi kwani kwa kukamilika kwabarabara hiyo kutakuza uchumi wa maeneo ya Wilaya ya Tunduru.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Ester Riwa amewashauri vijana hao kuweka itikadi za siasa pembeni kwani serikali yao hushirikiana vijana wote bila ubaguzi wa dini au kabila.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »