Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania Mh.Anna Makinda akimkaribisha
Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi katika viwanja vya Bunge mjini
Dodoma ambapo Rais huyo alilihutubia Bunge hilo.
Rais
Wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akipokea heshima muda mfupi baada ya
kuwasili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma akisindikizwa na mwenyeji
wake Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais
wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo huku Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Spika Mhe.Anna Makinda wakishuhudia.
Rais
Wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akilihutubia Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma huku Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete na Spika wa Bunge hilo Mh.Anna Makinda wakisikiliza.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto
Nyusi,Waziri Mkuu Mizengo Pinda,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na viongozi waandamizi katika serikali ya Msumbiji wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya Rais wa Msumbiji kulihutubia Bunge
lao mjini Dodoma(Picha na Freddy Maro)
EmoticonEmoticon