PETER TINO, ZAMOYONI MOGELLA NA WENGINE KIBAO KATIKA 'SEND OFF' YA RAIS KIKWETE JANA DAR

October 13, 2015


Washambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Zamoyoni Mogella (kulia) na Peter Tino kushoto wakifurahi pamoja katika sherehe ya Wanamichezo kumuaga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete anayemaliza muda wake mwishoni mwa mwezi huu iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA) jana ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam. Mogella alicheza kwa muda mrefu zaidi Yanga SC, wakati Tino alicheza zaidi Majimaji ya Songea.
Rais Kikwete akiteremka ngazi jana baada ya kuhutubia
Mwandishi wa Habari Athumani Hamisi alikuwepo kwenye sherehe hizo jana
Maofisa wa Bosi ya Ligi, Fatuma na Rose walikuwepo jana
Kutoka kulia Nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Nsajigwa Shadrack, kipa wa zamani wa Yanga SC, Stephen Malashi na kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa
Mchambuzi wa soka wa Azam TV, Jeff Leah (kulia) akiwa na Farough Baghozah, mmiliki wa kampuni ya TSN
Mkurugenzi wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga alikuwepo jana
Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto (kulia) akimuonyesha kitu Nahodha wa Taifa Stars, Nadir Haroub 'Cannavaro'
Arafat Bakari naye alikuwepo jana katika sherehe hizo
Mabondia wa zamani, Emmanuel Mlundwa (kulia) na Anthiny Lutta kushoto
Mwandishi wa Habari, Asha Kigundula (kushoto) na mumewe
Zaituni Kibwana (kulia) na Sofia Komba (kushoto)
Yassi Ustadh kulia na wanafamilia wenzake wa ndondi
Alhaj Mintanga naye alikuwepo pia kwenye sherehe hizo
Iddi Mshangama (kushoto) na Kalambo kulia walikuwepo pia jana
Beki wa zamani wa Simba SC, Mohammed Bakari 'Tall' alikuwepo pia jana
Jamal Rwambow kushoto na wadau wengine jana
Waandishi nguli, Grace Hoka na Zena Chande walikuwepo pia jana
Mwani Nyangassa na Majuto Omary walikuwepo pia jana

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »