MAMA SAMIA GEITA VIJIJINI NA MJINI

October 13, 2015

6
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananch baada ya kuwasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Oktoba 12, 2015, kwenye Viwanja vya Nyawilimilwa, jimbo la Geita Vijijini mkoani Geita. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita ambaye pia ni Mgombea Ubunge wa jimbo hilo, Joseph Kasheku maarufu kwa jina la King Msukuma.
2
Mgombea Ubunge jimbo la Geita Vijijini ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita, Joseph Kasheku ‘King Msukuma’ akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Nyawilimilwa, jimbo la Geita Vijijini mkoani Geita, Oktoba 12, 2015.
9
William Mabula aliyekuwa Mgombea Ubunge jimbo la geita mjini kwa tiketi ya Chadema, lakini chama hichi kikamuengua dakika za mwisho baada ya kushinda kura za maoni kisha kupachikwa mwingine aliyehamia chama hicho kutoka CCM, akitangaza kuhamia CCM wakati wa mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika jimbo hiko mkoani Geita, jana, Oktoba 12, 2015.
7
Mgombea Ubunge jimbo la Geita mjini, Costantine Kanyasu, akiomba kura wakati wa mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, katika jimbo hilo mkoani Geita, jana, Oktoba 12, 2015.
3
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassa, akimuonyesha tukio la kufurahisha, Mjumbe wa Kamati ya kampeni za CCM, Christopher Ole Sendeka, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Oktona 12, 2015, kwenye Viwanja vya Nyawilimilwa, jimbo la Geita Vijijini mkoani Geita.
12
5   8
Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Geita mjini mkoani, Geita.
10
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva anayeko katika kundi la Nimestuka, Juma Kiroboro maarufu kwa jina la Juma Nature, akishambulia jukwaa akiwa na Ispekta Haruna wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, uliofanyika jana, Oktoba 12, 2015, katika jimbo la Geita mjini mkoani Geita.
11
Msanii Ashura Mohammed, aliyeko katika kundi la Nimestuka, akionyesha umahiri wake wa kucheza muziki, wakati kundi hilo lilipoburudisha wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana, Oktoba 12, 2015
Picha na Bashir Nkoromo

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »