Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodrigues (kushoto)
akimkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine
Mushy msaada wa Vifaa vya mawasiliano (Cameras, printers na Computers)
kwa ajili ya kitengo cha Mawasiliano ya Serikali cha Wizara ya Mambo ya
Nje.
Balozi Celestine Mushy, akizungumza na Bw.
Alvaro Rodrigues muda mfupi kabla ya makabidhiano ya vifaa hivyo
kufanyika. Balozi Mushy alishukuru msaada huo ambao alisema umekuja
wakati mwafaka ambapo Serikali ipo katika mikakati ya kuboresha
mawasiliano na wadau wake.
Mazungumzo yakiendelea....
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy, akisaini nyaraka ya
makabidhiano kama ishara ya kupokea msaada huo.Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Bw. Alvaro Rodrigues naye akiweka sahihi kweye nyaraka ya makabidhiano kama ishara ya kukabidhi rasmi msaada huo wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya kitengo cha mawasiliano ya serikali cha Wizara ya Mambo ya Nje.
Balozi
Celestine Mushy akiwa ameshikilia moja ya vifaa vya msaada huo huku
baadhi ya Maofisa kutoka Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
wakishuhudia.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Mindi Kasiga, akipokea msaada huo
kutoka kwa Balozi Mushy.
Balozi Mushy akiwa ameshikilia Video Camera iliyotolewa msaada na UNDP.
PICHA NA: REUBEN MCHOME.