WAGANDA WAMSHANGAA ZARI KUMGANDA DIAMOND

December 06, 2014

Mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya Uganda vimemgeuka nyota wa vipindi vya runinga na Mwanamuziki Zari ‘The Boss Lady’ kwa madai kwamba amemganda mwanamuziki wa Tanzania Diamond Platnumz.
Gazeti la udaku la Red Pepper, mitandao ya ugvision.com, bigeye.ug na mingineyo, imedai kuwa nyota huyo amemganda mwanamuziki huyo tangu alipopata upenyo wa kurekodi naye singo jijini Dar es Salaam.
Mitandao hiyo ilimshambulia Zari kwa kumwambia kuwa kavuruga uhusiano baina ya Wema na mkali huyo wa video ya ‘Ntampata Wapi’, huku ikiponda picha ambayo Zari aliiweka mitandaoni ikimwonyesha akiwa na Diamond.
Mitandao hiyo imeponda kuwa Zari ana tabia ya kuwanadi wanaume anaotoka nao.
Wiki tatu zilizopita Zari amekuwa bega kwa bega na mwanamuziki Diamond, baada ya kutengeneza wimbo wa pamoja katika studio za Tuddy Thomas. Zari alionekana akipiga picha kadhaa na nyota huyo kabla ya kumsindikiza katika tuzo za CHOAMVA, Afrika Kusini na baadaye kurudi naye nchini.

Diamond ambaye alinyakua tuzo tatu za Channel O 2014, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla inayoandaliwa na Zari, ijulikanayo kama ‘Zari All White Ciroc Party’, itakayofanyika Desemba 18, mwaka huu.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »