Serikali imeahidi kuendelea kusaidia kuwajengea Vijana uwezo wa kujitambua na kufanya kazi kwa hari ikiwemo kujitolea.
Hayo yamebainishwa katika Hotuba
ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara
iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana
wakati wa hafla ya madhimisho ya Siku ya Kimataifa yakujitolea
iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Akihutubi baadhi ya Vijana
wanaofanya kazi za Kujitolea katika taasisi mbalimbali Kajugusi amesema
vijana wanapaswa kufanya kazi za kujitolea ili kujenga uwezo wa utendaji
kazi na kupata uzoefu utakaopelekea kuajirika kwa ulahisi.
“Jengeni tabia ya kujitolea kwa
kuwa kutawajenga na kuwapa fursa kubwa ya kupata ajira zenye staha
zitakazo kidhi matarajio yenu”
Aidha Mkurugenzi huyo alitoa rai kwa vijana kujunga tabia ya kujifunza na kutumia kwa manufaa yao na taifa kwa jumla wake
Kajugusi aliongeza kuwa Serikali
ipo mbioni kuboresha mkakati wa Taifa wa kushirikisha Vijana katika
shughuli za maendeleo hapa nchini ambapo vijana watapa fursa ya
kushiriki moja kwa moja katika kutekeleza mipango ya maendeleo ya nchi
yao.
Kwa upande wake Afisa Habari wa
Kituo cha Habari cha Umoja wa Matifa (UNIC) Bibi. Stella Vuzo amesema
kuwa kadri vijana wanavyofanya kazi za kujitolea ndipo wanapopata fursa
ya kujijengea uwezo utakapoelekea waajirike katika sjira zenye staha
Aliongeza kuwaidi ya vijana
asilimia 80 wanajitolea katika taasisi mbalimbali duniani kote, ambapo
kati yao asilimia 30 ujitolea ndani ya nchi zao hivyo kusaidia kuongeza
nguvu kazi katika shughuli za maendeleo.
Akisoma ujumbe mahususi wa Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwa ajili ya maadhimisho hayo,
Bibi. Vuzo alisema kuwa Katibu Mkuu huyo anawashukuru zaidi ya watu
6,300 wanaofanya kazi kwa kujitolea katika Umoja wa Mataifa na na 11,000
wanaojitolea kupitia Mtandao kwa kuweza kuwasidia zaidi ya mamilioni ya
watu katika kufanya mabadiliko kwa kuwapa sauti katika maendeleo
endelevu na jitihada za utunzaji wa amani duniani kote’Alisema Stella
Vuzo.
Siku ya Kujitolea duniani
uadhimishwa kila mwaka tarehe 5 Desemba duniani kote ambapo kwa Tanzania
kitaifa maadhimisho haya yamefanyika jijini Dar es Salaam
EmoticonEmoticon