Michuano ya Taifa ya mpira wa
miguu kwa wanawake ya Proin Women Taifa Cup inaanza rasmi Desemba 28
mwaka huu kwa mechi ya ufunguzi kati ya timu za mikoa ya Mara na Mwanza
itakayochezwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kombaini za mpira wa miguu za
mikoa yote ya Tanzania Bara zitashiriki mashindano hayo yatakayochezwa
kwa raundi mbili mwanzoni, na baadaye hatua ya robo fainali hadi
fainali.
Mashindano hayo yanayodhaminiwa na
kampuni ya Proin Promotions Limited, kuanzia hatua ya robo fainali,
mechi zote zitafanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja Biashara wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania, Peter Simon Shankunkuli aliishukuru kampuni ya
Proin ambao ni watengenezaji, wazalishaji na wasambazaji wa filamu za
kitanzania kwa kuwezesha mashindano hayo kufanyika kwa mara ya kwanza
Proin Promotions imekua ikivumbua
vipaji mbalimbali vya uigizaji na sasa imeamua kujikita katika mpira wa
miguu ili kuweza kuvumbua vipaji kwa wachezaji wa kike.
Shankunkuli alisema nafasi bado
zipo kwa wadhamini watakaoguswa na mashindano hayo, kwa kuwasiliana na
TFF au Proin Promotions Limited kwa maelezo zaidi.
EmoticonEmoticon