Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya Bw. Khamis Mdee akipokea tuzo tuzo tatu za ubunifu
katika sekta ya hifadhi ya Jamii Barani Afrika zinazosimamiwa na
Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Duniani (ISSA)
katika sekta ya hifadhi ya Jamii Barani Afrika zinazosimamiwa na
Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Duniani (ISSA)
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya Bw. Khamis Mdee
katikati akionyesha tuzo hizo pamoja na washiriki we ngine wa mkutano
huo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya Bw. Khamis Mdee na washiriki wengine wakiwa katika mkutano huo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya Bw. Khamis Mdee akiwa na maofisa wengine wa mfuko huo wakiwa katika picha ya pamoja.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya Bw. Khamis Mdee na
washiriki wengine kutoka mataifa mbalimbali wakiwa katika mkutano huo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya Bw. Khamis Mdee akielezea jambo katika mkutano huo.
Mandhari ya jiji la Cassablanca Morocco
……………………………………………………………………………………………….
Mwandishi Maalum Casablanca, Morocco
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF umenyakua tuzo tatu za ubunifu katika sekta ya hifadhi ya Jamii Barani Afrika zinazosimamiwa na Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Duniani (ISSA).
Halfa ya kukabidhi tuzo hizo ilifanyika Jijini Casablanca nchini
Morocco usiku wa tarehe 3 Desemba, 2014 katika hoteli ya Serana jijini Casablanca ambapo washiriki zaidi ya 360 kutoka taasisi 75 katika mataifa 45 ya Afrika zilihudhuria.
Tuzo ambazo NHIF ilikabidhiwa ni katika eneo la utoaji wa huduma zamatibabu za kibingwa maeneo magumu kufika, kazi ambayo mfuko umefanyakwa kushirikiana na wataalamu wa hospitali za rufaa nchini.
tuzonyingine ni katika eneo la TEHAMA katika utayarishaji madai na hudumaza matibabu kwa wanachama wastaafu.
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo wa Kanda ya Afrika ambacho piakilijadili mambo muhimu kuhusu sekta ya hifahi ya jamii na kutambuakazi za ubunifu uliongozwa na Waziri wa kazi Mheshimiwa GaudensiaKabaka pamoja na Viongozi waandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi naUdhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii nchini (SSRA) na baadhi ya
Watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini.
Tangu kuanza kutolewa kwa ambazo hushindaniwa kila baada ya miakamitatu, NHIF imeng’ara mara zote.Mwaka 2008 ilipata tuzo ya cheti chaheshima cha ubunifu mjini Kigali kwa kuwashirikisha wadau wake katikautoaji wa elimu kwa makundi mbalimbali ngazi ya mkoa. Mwaka 2011ulikuwa mshindi wa kwanza wa jumla barani Afrika na mwaka huu umeibuka tena na ushindi huo muhimu unaoitangaza Tanzania kimataifa kupitia Bima ya Afya.
Mbali ya NHIF, Tanzania pia imengara kwa kuzoa jumla ya tuzo 6 mbapoMamlaka ya Udhibiti ya SSRA, Mfuko wa Pensheni wa PPF na Mfuko wa PSPSpia ilijizolea tuzo moja moja kwa kila mmoja hivyo kufanya Tanzaniakuwa na jumla ya tuzo 6 na kuifanya kuwa kinara katika ukanda wa nchiza Afrika mashariki na ya Kati.
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika nchi nne ilipata heshima ya pekeekwa kazi zao za ubunifu. Mifuko hiyo ni kutoka Cameroon yenyewe
iliyonyakua tuzo 8, Gabon, Maurtania, wenyeji Morocco.
Washindi wa jumla wa kwa mwaka 2014 ni wenyeji Morocco na Jirani zaowa Mauritania ambao kwa pamoja wamepata tuzo ya jumla kwa kutoa huduma bora, kuongeza uwigo wa wanaonufaika na huduma za mifuko hiyo hasa wasio na uwezo, matumizi ya TEHAMA na huduma kwa wateja na ufanisi kwa
ujumla.
EmoticonEmoticon